Posts
Showing posts from April 17, 2026
Jiji la Dodoma latumia Mil. 29 miundombinu S/M Ihumwa B
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Mwandishi Wetu, IHUMWA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa kiasi cha shilingi 29,000,000 kwaajili ya umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa ya Shule ya Msingi Ihumwa B, hatua inayosaidia kuimarisha mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Hayo aliyasema Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ihumwa B, Mwl. Daudi Mwakalinga wakati alipokuwa akisoma taarifa mbele ya Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2025/2026. Alisema kuwa fedha hizo zilipeleka mabadiliko chanya shuleni hapo. “Kupitia fedha hizi, shule imefanikiwa kuboresha madarasa, hali iliyochangia kuongeza hamasa kwa walimu na wanafunzi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji” alisema Mwl. Mwakalinga. Pia, alitoa shukrani kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwapatia fedha hizo kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule. “Tunatoa shukrani za dhati...