Mkuu wa Wilaya Dodoma aagiza ujenzi Fensi maeneo ya wazi Nkuhungu
Na. Mwandishi wetu, NKUHUNGU Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ameagiza maeneo yote ya wazi katika Kata ya Nkuhungu kuwekwa fensi ili kuyakinga dhidi ya uvamizi na matumizi yasiyo sahihi, ikiwemo uuzaji holela wa maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma. Alhaj Shekimweri alitoa agizo hilo alipofanya ziara katika Mtaa wa Bochela kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabwawa yanayolenga kudhibiti maji ya mvua na kupunguza athari za mafuriko katika makazi ya wananchi. Alisema kuwa ulinzi wa maeneo ya wazi ni muhimu katika kuhakikisha yanabaki kwa matumizi yaliyokusudiwa na kuzuia watu kuyavamia au kuyagawa na kuuziana kinyume cha taratibu, hali ambayo inaweza kuathiri mipango ya maendeleo kwa siku zijazo. “Kila eneo la wazi katika kata hii liwekewe fensi ili kuzuia uvamizi na watu kuuziana maeneo ya wazi, hali ambayo inaweza kuleta changamoto baadaye,” alisema Alhaj Shekimweri. Aidha, alisema kuwa uwekaji wa fensi utasaidia kulind...