Posts

Showing posts from December 28, 2024

Usafi mwisho wa Mwezi waendelea Kata ya Mnadani

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Wananchi wa Kata ya Mnadani Halmashauri ya Jiji la Dodoma walifanya usafi wa mazingira mita tano kuzunguka maeneo yao ya makazi na biashara ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la usafi, Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Usimamizi wa Taka ngumu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro, alisema kuwa ni wajibu wa viongozi kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kufanya kazi kwa pamoja na wananchi. Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na utupaji wa taka ovyo katika maeneo na kufanya usafi katika mitaro ambayo inapitisha maji machafu kipindi hiki cha mvua nyingi na kujiepusha na mafuriko yatokanayo na uzibaji wa mitaro. “Usafi ni ustaarabu ambao unaanza na mimi na wewe. Lakini katika kipindi hiki cha masika, kumekuwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali ya kuhara na kutapika ambayo tunaweza kujiepusha kwa kufanya usafi kwenye maeneo yetu” alisema Kimaro...