BARAZA LA MADIWANI JIJI LA DODOMA LAMSHUKURU RAIS SSH

Na. Dennis Gondwe, DODOMA BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma linamshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa katika jiji hilo kwa kusimamia ubora na thamani ya fedha. Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akimshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe katika mkutano wa baraza hilo wa kuwasilisha taarifa za maendeleo kutoka kwenye kata uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya jiji hilo. Prof. Mwamfupe ambae ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa halmashauri yake inaweka msisitizo katika kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. “Sisi Jiji la Dodoma tunawiwa kumshukuru Mheshimiwa Rais, kwa sababu ni wanufaika wakubwa wa miradi inayotoka serikali kuu. Shukrani zetu kubwa zaidi ni usimamizi wa miradi, ku...