Posts

Showing posts from April 29, 2026

OFISI ZA KANDA ZASOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI DODOMA

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Jiji la Dodoma lilianzisha Kanda Saba kwaajili ya kusogeza huduma kwa wananchi lakini lengo kuu likiwa ni kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri ambayo yanatumika katika kuleta maendeleo kwa jamii. Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi zilifanyika kwa kipindi cha robo ya tatu, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula alisisitiza umuhimu wa matumizi ya mfumo wa kanda katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kubuni vyanzo vipya na kuviimarisha vilivyopo. Alisema kuwa mfumo wa kanda umeendelea kutoa mafanikio makubwa kwa kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, kuimarisha usimamizi wa vyanzo vya mapato na kuongeza uwajibikaji kwa wataalam waliopo katika maeneo husika. "Katika kipindi cha robo ya tatu, matumizi ya mfumo wa kanda yamesaidia kuongeza ufuatiliaji wa karibu wa vyanzo ...

KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KUTOA ELIMU YA KINGA KWA VIJANA DODOMA

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Kamati ya Kuzuia na Kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya DOYODO imeendelea kutoa elimu na mafunzo kwa jamii, hususan kwa vijana, ili kuhakikisha wanapata uelewa sahihi wa namna ya kujikinga na ugonjwa huo. Hayo aliyasema Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma (WASEMI), Leticia Sanga tarehe 29 Aprili, 2026 wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kudhibiti UKIMWI kwa kipindi cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi, 2026 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda, lakini bado kuna haja ya kupanua wigo wa elimu hiyo. “Tumekuwa tukiwalenga zaidi vijana, lakini sasa tumeona umuhimu wa kuwafikia pia wazee. Wazee wengi wamekuwa waathirika wakubwa wa janga hili kwa sababu wanabeba jukumu la kuwahudumia watoto wao wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Hivyo, nao wanahitaji elimu hii kwa kina zaidi” al...

DODOMA YAADHIMISHA MIAKA 62 YA MUUNGANO, DC SHEKIMWERI ASISITIZA AMANI NA MSHIKAMANO

Image
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Alhaji Jabir Mussa Shekimweri, ameongoza kilele cha maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika Shule ya Msingi Nane Nane, Kata ya Nzuguni, akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na mshikamano ili kuchochea maendeleo endelevu ya Taifa. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Alhaj Shekimweri alisema kuwa kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Miaka 62 ya Muungano: Amani, Umoja na Mshikamano ni Msingi wa Maendeleo Endelevu” inapaswa kila Mtanzania aiishi kwa vitendo. Alieleza kuwa mafanikio ya taifa yanategemea mshikamano wa wananchi wake, akisisitiza umuhimu wa kulinda amani na kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia maendeleo ya kweli na ya kudumu. “Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuilinda amani, kuimarisha umoja na mshikamano kwasababu hayo ndiyo msingi wa maendeleo endelevu ya nchi yetu. Aidha, tujishughulishe na shughuli za kiuchumi ili kujikwamua na kuinua hali zetu za maisha” alise...

WAKAZI WA NALA WAADHIMISHA MIAKA 62 YA MUUNGANO KWA KUSHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA

Image
Na. Mwandishi Wetu, NALA - DODOMA WAKAZI wa Mtaa wa Barazani, Kata ya Nala wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa mazingira linalofanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa lengo la kuendelea kuhakikisha mji unakuwa safi na kujenga mazoea ya kupenda kufanya usafi. Zoezi hilo la usafi limekuwa la kipekee kwasababu limefanyika sambamba na kuadhimisha Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo wananchi walionekana wenye hamasa kubwa katika kuboresha muonekano wa mtaa wao. Akizungumza na wakazi ho mara baada ya zoezi la usafi kukamilika, Afisa Mazingira kutoka Kanda Namba Tatu, Neema Komba aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kuonesha uthamani wa kuishi katika mazingira safi. “Leo tumefanya jambo jema sana kujitokeza kufanya usafi, kwanza tumetimiza ule wajibu wetu wa kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi lakini pia tupo hapa kuadhimisha kwa umoja wetu miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano huo unaendelea kutukumbusha kus...

KANDA NAMBA MBILI YAADHIMISHA MIAKA 62 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KWA KUFANYA USAFI WA JUMAMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI

Image
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA KANDA Namba Mbili imeadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya zoezi la usafi katika Kata ya Nzuguni, Mtaa wa Nzuguni A pamoja na Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuenzi umoja na mshikamano wa watanzania. Zoezi hilo liliongozwa na Meneja wa Kanda Namba Mbili, Hussen Nyenye aliyeshirikiana na watumishi wa kanda hiyo pamoja na wananchi kusafisha mazingira katika maeneo hayo muhimu ya jiji. Akizungumza wakati wa zoezi hilo aliwashukuru Kikundi cha Wanawake wa Stendi maarufu kama Malkia wa Nguvu kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki usafi huo. “Nawapongeza sana Malkia wa Nguvu kwa kuungana nasi kusafisha eneo hili muhimu ikiwa ni moja ya njia za kuadhimisha muungano wetu huku tukizingatia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo ‘Miaka 62 ya Muungano: Amani, Umoja na Mshikamano ni Msingi wa Maendeleo Endelevu'. Pia tukumbuke kuwa mazingira safi ndiyo msingi wa kila kitu katika maendeleo ya jamii” alisema Nyenye. Kwa up...

Kanda Namba Moja yaadhimisha Miaka 62 ya Muungano kwa kufanya Usafi

Image
  Viongozi wa Kanda Namba Moja, viongozi wa kata na mitaa pamoja na wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, wameungana kushiriki zoezi la usafi katika Kata ya Uhuru kwa kusafisha mitaro ya maji ya mvua iliyopo kando ya barabara. Zoezi hilo limefanyika kwa lengo la kuimarisha usafi wa mazingira na kuhakikisha usalama wa afya za wananchi. Aidha, zoezi hilo lilifanyika ikiwa sehemu ya maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yenye kaulimbiu isemayo: "Miaka 62 ya Muungano: Amani na Mshikikamano ni Msingi wa Maendeleo Endelevu". Kupitia zoezi hilo, wananchi walikumbushwa umuhimu wa kudumisha usafi wa mazingira kila siku, bila kusubiri usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi au wakati wa maadhimisho ili kujenga jamii yenye afya bora na maendeleo endelevu.