Shule ya Msingi Chinangali wapewa elimu ya Uzalendo

Na. Leah Mabalwe, CHAMWINO Wanafunzi wa shule ya Msingi Chinangali Kata ya Chamwino wapewa elimu juu ya uzalendo wa nchi yao. Hayo yalijili baada ya Afisa Ushilikishwaji wa Jeshi la Polisi Kata ya Chamwino, A/Insp Isiaka Shabani kutembelea shule hiyo na kutoa mafunzo ya uzalendo na kusema kuwa kila wanafunzi ni jukumu lake kuwa mzalendo. “Kila mwanafunzi ni jukumu lake kuwa mzalendo na kuachana na matendo mabaya ambayo yanajikita katika ukatili na badala yake kuwa mzalendo katika Taifa lake kwa kumtolea mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan” alisema A/Insp. Shabani. Aidha, aliongeza kwa kuwataka wanafunzi hao kujua umuhimu wa Bendera ya Taifa maana yake hususani rangi zinazopatikana katika Bendera ya Taifa ni kielelezo kikubwa cha Taifa. Pia alimalizia kwa kuwasihi wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Chinangali kuwa inapaswa kuwa mzalendo popote pale watakapo kuwepo na uzalendo huanzia ndani ya moyo wa mtu na kila Mtanzania n...