Posts

Showing posts from October 17, 2023

JIJI LA DODOMA LATAMBUA JITIHADA ZA MWANAMKE WA KIJIJINI

Image
Na. Dennis Gondwe, CHIHANGA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inatambua jitihada zinazofanywa na mwanamke wa kijijini katika uzalishaji wa chakula na kusimamia lishe ya familia. Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Charity Sichona Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Charity Sichona alipokuwa akiongea maadhimisho ya siku ya mwanamke anayeishi kijijini ofisini kwake leo ambayo yatafanyika katika Kata ya Chihanga jijini Dodoma. Sichona alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaadhimisha siku hiyo kwa lengo la kuendelea kutambua jitihada za mwanamke anayeishi kijijini. ā€œWanawake wanaoishi vijijini wanamchango mkubwa katika kuzalisha chakula na kuchangia uwepo wa chakula katika familia na nchi nzima. Hivyo, serikali imeamua kutambua jitihada zao za kilimo, ufugaji na shughuli za kiuchumi na kuwatia moyo ili waendelee kuzalisha wakati serikali ikiendelea kutatua changamoto zinawakabiliā€ alisema Sichona. Sichona alisema ku...

WASIMAMIZI KLINIKI YA ARDHI WATAKIWA KUJALI MAKUNDI MAALUM

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WASIMAMIZI wa Kliniki ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kutoa kipaumbele kwa makundi maalum yanapokwenda kupata huduma katika kliniki hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akiongea na waandishi wa habari Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabr Shekimweri alipokuwa akiongea na waandishi wa habari alipotembelea Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika siku yake ya pili jijini hapa ya kutatua migogoro ya Ardhi. Shekimweri alisema ā€œniwaombe sana, mkusanyiko huu una watu mchanganyiko wapo wa umri wa kati, watu wazima, wazee, wenye changamoto za malazi, wajawazito na wenye ulemavu. Pamoja na utaratibu uliopangwa tuheshimu mahitaji ya haya makundi maalumā€ alisema Shekimweri. Aidha, aliwataka wananchi wanaokwenda kupata huduma katika kliniki hiyo kwenda na nyaraka kamili ili kuwasaidia wataalam katika kutatua kero za ardhi. ā€œWakati wa kuwasilisha changamoto na kero tujitahidi kuja tukiwa tumekamilisha nyaraka za...

JIJI LA DODOMA LAPONGENZWA KLINIKI YA ARDHI ILIYOWATOA WATAALAM OFISINI KUHUDUMIA WANANCHI

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kuanzisha Kliniki ya Ardhi iliyowafanya wataalam kutoka ofisini na kuweka kambi kuwahudumia wananchi eneo moja ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akiongea na waandishi wa habari katika Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo eneo la Manispaa ya zamani alipotembelea na kukagua maendeleo ya Kliniki ya Ardhi inayotoa huduma jijini hapa. Shekimweri alisema ā€œkipekee nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, niliyasema haya wakati tunakupokea hapa Dodoma baada ya kuteuliwa. Mimi nakufahamu unavyofanya kazi. Ninafahamu ni mtu unaejali sana watu na matatizo ya wananchi. Nilikuwa nawaambia wananchi ninajua kuna mkurugenzi atawasilikiza kwa nafasi na kwa staa na atawashughulikia matatizo yenu yaliyowasumbua kwa muda mrefuā€. Alisem...

JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA MBADALA 1,105 KWA WANANCHI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa viwanja mbadala 1,105 kwa wananchi katika kutekeleza mkakati wake wa kumaliza migogoro ya Ardhi jijini hapa. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo akongea na waandishi wa habari Mamia ya wananchi wakiwa katika mahema kupata huduma katika Kliniki ya Adhi Jiji la Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya pili ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini hapa. Kayombo alisema kuwa wakati anafika Dodoma kulikuwa na wananchi takribani 4,000 wanaodai viwanja mbadala. ā€œYaani kiwanja kimoja kimegawiwa kwa mwananchi zaidi ya mmoja. Lakini mpaka sasa tumeshatoa viwanja 1,105 kufidia wale wananchi. Mpaka sasa tunadaiwa viwanja 2,895. Matarajio mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka huu tutakiwa tumekamilisha kutoa viwanja hivyo 2,895. Kwa sababu kuna zoezi kubwa linaendelea la kupima eneo...

HATI 240 ZATOLEWA SIKU YA KWANZA YA KLINIKI YA ARDHI JIJINI DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA SIKU ya kwanza ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma yapokea wananchi 1,014 ikitoa Hati miliki 240 baada ya kusikiliza wananchi 514. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo akiongea na waandishi wa habari kuhusu siku tano za Kliniki ya Ardhi katika Jiji la Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Kliniki ya Ardhi iliyoanza siku ya pili katika jiji hilo kutatua migogoro ya Ardhi. Kayombo alisema kuwa siku ya jana walipokea wananchi 1,014. ā€œWananchi tuliofanikiwa kuwasikiliza jana ni 514. Katika wananchi 514 tumefanikiwa kutoa Hati 240. Tulifanikiwa kusikiliza watu wenye migogoro 209. Wale waliobaki jana tumeendelea nao leo asubuhi. Leo watu ni wengi kuliko jana na wameshapewa namba na huduma zinaendelea vizuriā€ alisema Kayombo. Akiongelea matarajio ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa ni kutatua migogoro ya Ardhi...