Posts

Showing posts from May 15, 2025

Bima ya Taifa ya Afya yatoa huduma kieletroniki

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Maboresho ya huduma ya Bima ya Afya yamefanywa kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia ambapo wananchi wanaweza kujisajili kupata huduma za bima kupitia simu zao na vifaa vya kieletroniki vyenye ‘Internet’. Hayo yalisemwa na Afisa Wanachama Mwandamizi, Bima ya Afya Mkoa wa Dodoma, Bakary Hamdun katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri wakati akiwasilisha sheria ya afya na kanuni zake. Alisema kuwa kila mwanachama anaetarajia kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) anaweza kujihudumia kupitia simu ya mkononi “Mwanachama yeyote awe mtumishi au mwananchi wa kawaida anaweza kujisajili kupitia simu yake ya mkononi. Na anaweza kufanya hivyo bila kuwa na changamoto ya aina yoyote kwasababu huduma hii ni rahisi pia inafanyika kwa muda mfupi” alisema Hamdun. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe aliipongeza serikali kwa hatua kubwa ya uboresha...