WIZARA YA ARDHI KUBORESHA MFUMO WA ILMIS

Na. Dennis Gondwe, DODOMA WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kuboresha mfumo wa kieletroniki wa kutunza taarifa za Ardhi (ILMIS) ili kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa hati milki ikiwa niutekelezaji maelekezo ya serikali. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa akiongea na waandishi wa habari Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dodoma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Slaa alisema “tarehe 3 Oktoba, 2023 serikali ilitoa maelekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Maelekezo hayo yalihusu mamlaka mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa sekta ya Ardhi. Wizara inaendelea na uboreshaji wa mfumo wa kieletroniki wa kutunza t...