Posts

Showing posts from May 27, 2026

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lawafukuza kazi watumishi watatu na mmoja kushushwa cheo

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limewafukuza kazi watumishi watatu na mtumishi mmoja kushushwa cheo na mshahara kufuatia kukiuka misingi na taratibu za Utumishi wa Umma. Maamuzi hayo yalifanyika katika Mkutano maalum wa Mashauri ya Kinidhamu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Watumishi waliofukuzwa kazi ni Afisa Muuguzi Msaidizi, Muuguzi na Afisa Mtendaji wa Mtaa. Mtumishi aliyeshushwa cheo na mshahara ni Mteknolojia Maabara. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula alilihoji Baraza la Madiwani, na kwa kauli moja liliridhia kuwafukuza kazi watumishi hao watatu na kushushwa cheo na mshahara mtumishi mmoja. Akiwasilisha taarifa ya kuhitimisha mashauri ya nidhamu ya watumishi wanne kwa Baraza maalum la Mashauri ya Nidhamu, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Gerald Ruzika alisema kuwa mkurugenzi aliunda kam...

Kimaro: Wananchi Dodoma waalikwa kuupokea Mwenge wa Uhuru Juni, 1 2026

Image
  Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula katika maandalizi ya Mwenge wa Uhuru 2026 Wilaya ya Dodoma, Dickson Kimaro anawaalika wananchi kushiriki mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwakumbusha kuwa tukio hilo linawaungansha pamoja na kujenga mshikamano wa kimaendeleo. Mwenyekiti wa Kamati ya huduma ya Chakula Wilaya ya Dodoma Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma unaotarajiwa kuwasili tarehe 1 Juni, 2026 na kukimbizwa katika miradi saba ya maendeleo. Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri. “Maandalizi mpaka leo hii yapo vizuri na Kamati ya Chakula imejipanga katika eneo la chakula kwa kuhakikisha wote wanaohudhuria wanapata chai itakayotolewa katika Shule ya Sekondari, Dkt. Samia na chakula cha mchana kitakuwepo pale katika Shule ya Sekondari Umonga. Chakula cha usiku kitapatikana katika shule ya Msingi Kizota’’ alisema Kimaro. Kimaro ambae pia ni Mkuu wa...

Odero: Mwenge wa Uhuru alama ya Umoja Wilayani Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wa Wilaya ya Dodoma wameombwa kuonesha umoja na mshikamano wao kwa kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru utakapowasili na kutembelea miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha yao. Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero akionesha utayari wa kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Vincent Odero alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma. Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ni chombo cha umoja na mshikamano ambao umekuwa ukitafsiriwa kwa vitendo wilayani Dodoma. “Wilaya ya Dodoma tumekuwa tukionesha umoja na mshikamano wa wazi linapokuja suala ya Mwenge wa Uhuru kwa miaka yote. Hili ni jambo la heshima kwetu. Nitumie nafasi hii kuwaalika na kuwaomba tena wananchi wote tarehe 1 Juni, 2026 kuupokea Mwenge wa Uhuru katika Mtaa wa Vikonje B, Kata ya Mtumba n...