Posts

Showing posts from July 17, 2026

Wananchi Kata ya Chang’ombe wahimizwa kulinda miundombinu

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wananchi wa Kata ya Chang’ombe watakiwa kuendelea kuitunza na kuilinda miradi ya maendeleo ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu na kuvinufaisha vizazi vya sasa na vijavyo. Hayo aliyasema Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Bakari Fundikira mara baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata ya Chang’ombe jijini Dodoma. Alisema kuwa serikali imeendelea kuwekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma za kijamii na kuinua ustawi wa wananchi. “Hivyo, ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika kuilinda na kuitunza. Leo tumetembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Kishoka, Ofisi ya Mtaa wa Chang’ombe Juu, Ofisi ya Mtaa wa Hamvu, kisima cha maji Shule ya Msingi Chang’ombe na ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Chang’ombe ambapo miradi hii imejengwa kwa fedha za serikali jumla ya shilingi 456,926,355. Lakini pia nitoe rai kuwa ni m...

Usafi Jumamosi Tarehe 18 Julai, 2026

Image
 

Wataalam Ilemela MC wajifunza mfumo wa utenganishaji taka Dodoma Jiji

  Wataalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamefanya ziara ya mafunzo ya mbinu bora za usimamizi wa usafi wa mazingira hasa mfumo wa kutenganisha taka na kuona vihifadhio vinavyotumika kutenganishia taka katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Ziara hiyo ya mafunzo ilijifunza jinsi kampuni maalum ya kutekeleza miradi (SPV) ya halmashauri inavyotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na kutembelea miradi inayotekelezwa ya Bustani ya Mapumziko ya Chinangali na Duka kuuza vifaa vya ujenzi.

Jiji la Dodoma lajinoa kuelekea SHIMISEMITA 2026

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Timu ya Mpira wa Pete ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kujinoa kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA 2026 yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti, 2026 jijini Mbeya, mara baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Jamhuri kabla ya kuingia kwenye dimba la mashindano rasmi. Hayo aliyasema Afisa Michezo wa Jiji la Dodoma, Neema kilongola mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma Alisema kuwa michezo ya kirafiki ni sehemu muhimu ya maandalizi kwa kuwa husaidia kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi mapungufu hayo. "Lengo la mchezo huu wa kirafiki halikuwa kushinda pekee, bali ilikuwa ni kujipima uwezo wetu, kubaini mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi kabla ya kuanza mashindano ya SHIMISEMITA. Tunaendelea kujenga timu imara na tunaamini tutafika Mbeya tukiwa katika kiwango kizuri cha ushindani " alisema Kilongola. Aliongeza kuwa kikosi hicho kinaendelea na programu maalum za mazoezi zinazolenga ...