Hai DC kuimarisha miradi ya kimkakati baada ya kujifunza Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imejifunza mbinu za kubuni na kuendeleza miradi ya kimkakati baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Dodoma. Ziara hiyo ilihusisha Soko la Job Ndugai, Soko la Wazi la Machinga, Chinangali Park, maegesho ya malori Nala, Jengo la Kitenga Uchumi Mtumba pamoja na Kituo Kikuu Cha Mabasi Dodoma. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Edmund Rutaraka alisema kuwa ziara hiyo imewapa fursa ya kuona namna miradi mbalimbali inavyotekelezwa na kupata uzoefu wa kuboresha miradi katika halmashauri yao. “Tumejifunza umuhimu wa kuwa na maeneo maalumu kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo biashara, maegesho ya magari makubwa na huduma za usafiri, ili kuboresha huduma kwa wananchi kulingana na mahitaji yao,” alisema Rutaraka. Kwa upande wake, Diwani wa viti maalumu wa Tarafa ya Masama, Lightness Laizer alisema kuwa wamejifunza mbinu mbalimbali za kuende...