NHIF yaachana na utaratibu wa kusubiri wananchi ofisini
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wapongezwa kwa hatua ya kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kuwapatia elimu na huduma za afya, badala ya kusubiri wananchi wafike katika ofisi. Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabiri Shekimweri wakati wa uzinduzi wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili, Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika Soko la Wazi la Machinga. Alisema kuwa eneo hilo ni muhimu kwa kuwa linakutanisha makundi mbalimbali ya wananchi, wakiwemo wafanyabiashara, madereva na wananchi kwa ujumla. “Niwapongeze NHIF kwa kuchagua eneo hili la Machinga, ambalo lina wananchi wa makundi mbalimbali. Niwaombe muendelee na utaratibu huu wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao badala ya kukaa ofisini na kuwasubiri. Hii itasaidia wananchi wengi zaidi kufikiwa na kupata huduma” alisema Alhaj Shekimweri. Aliongeza kuwa hatua hiyo inaonesha umuhimu wa kusogeza huduma karibu na wananchi, hususan wale ambao...