Watumishi watakiwa kuzingatia nidhamu na mshikamano kazini
Na. Mwandishi Wetu, MAKOLE
Watumishi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kuzingatia
nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku lakini pia kuwa na
mshikamano na ushirikiano katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuboresha
utendaji kazi.
Hayo aliyasema Afisa Mtumishi Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Gerald Ruzika katika kikao cha kwanza cha Kamati Tendaji ya Wilaya ya Dodoma (TALGWU) kilichojadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Mei hadi Agosti 2026 kilichofanyika katika Ofisi ya Kata ya Makole.
Alisema kuwa nidhamu kazini ni msingi wa uwajibikaji
na utoaji wa huduma bora, huku ushirikiano baina ya watumishi ukiwa njia muhimu
ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto na kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa
majukumu yao. “Nidhamu katika kazi na mshikamano miongoni mwa watumishi ni
msingi wa utendaji wenye ufanisi. Tunapaswa kushirikiana katika kutatua
changamoto ili kuimarisha uwajibikaji na kuboresha huduma tunazozitoa” alisema
Dkt. Ruzika.
Aidha, amewahimiza watumishi kuendeleza utamaduni wa
kushirikiana, kuwasiliana kwa uwazi na kuwajibika katika maeneo yao ya kazi ili
kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Kikao hicho kimekuwa sehemu ya kupitia taarifa ya
utendaji kazi kwa kipindi husika, kujadili masuala ya kiutumishi na kuimarisha
ushirikiano katika kukabiliana na changamoto zinazoweza kuathiri utekelezaji wa
majukumu.




Comments
Post a Comment