Wanafunzi CBE wapatiwa elimu kujikinga na VVU

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

 

Elimu kuhusu kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) imetolewa kwa wanafunzi wa Chuo Elimu ya Biashara (CBE), ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa wa vijana kuhusu afya zao na kuwahamasisha kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo.

 


Daktari wa Kituo cha Afya Nkuhungu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Justa John, akizungumza na wanafunzi hao, ameeleza umuhimu wa kuwa na uelewa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI, pamoja na kufahamu njia mbalimbali za kujikinga na maambukizi.

 

Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao, kuzingatia njia salama za kujikinga na kuepuka vitendo vinavyoweza kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.

 

Aidha, ameeleza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya afya katika taasisi za elimu ili kuwajengea wanafunzi uelewa utakaowawezesha kujilinda na kulinda afya zao.

 


Kwa upande wake, Waziri wa Afya wa wanafunzi, Faustine Musoma, akizungumza kwa niaba ya wanafunzi, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuhamasisha vijana kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU na kuimarisha elimu ya afya katika mazingira ya vyuo.

 

Ameeleza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa wanafunzi kwa kuwa inawasaidia kuongeza uelewa, kufanya maamuzi yenye tija na kuwa mabalozi wa uhamasishaji wa afya kwa wenzao na jamii kwa ujumla.

Comments

Popular Posts

Vikundi vya Kata ya Kizota vyapatiwa elimu ya mikopo ya 10%

JIJI LA DODOMA LAJA NA TEKNOLOJIA YA NISHATI MBADALA MAONESHO YA NANENANE

Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za usafi wa Mazingira