Posts

Afisa Biashara Jiji la Dodoma aelezea umuhimu wa kuanzisha Kanda za Huduma

Image
Na. Ramla Makamba, HOMBOLO BWAWANI Katika kuhakikisha huduma za mapato zinapatikana kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanzisha mfumo wa kanda zitakazohudumia wakazi wa kata mbalimbali kwa karibu ambapo wataalamu watakuwa katika maeneo mbalimbali kutoa huduma hizo zikiwemo huduma za ukataji wa leseni ambapo mpango huo utaanza mapema mwezi Agosti, 2025. Wananchi watapata huduma kama vile za ulipaji wa tozo mbalimbali katika maeneo yao bila kulazimika kufuata huduma Katikati ya jiji ikiwa ni miongoni mwa harakati za kutatua changamoto za umbali wa upatikanaji wa huduma pamoja na kuhakikisha ukusanyaji thabiti wa mapato ya serikali ambapo mwanzoni yalikuwa hayafanywi kikamilifu. Hayo yalisemwa na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fikiri Mtoi, katika kikao kilichofanyika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani jengo la utawala, na kuhudhuriwa na watendaji wa kata, watendaji wa mitaa, wenyeviti wa mitaa na wadau wa b...

Wenyeviti Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani wapewa mafunzo huduma ndogo za kifedha

Image
Na. Rehema Kiyumbi, HOMBOLO BWAWANI Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma latoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Hombolo Bwawani juu ya matumizi ya fedha na kuweka akiba kwa lengo la kujikwamua kiuchumi. Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hidaya Abdallah alisema kuwa elimu ya huduma za kifedha ni muhimu kwa wananchi ili kuweza kufahamu namna ya kufanya matumizi na kuweka akiba. Alisema kuwa kikao hicho kimewahusisha wenyeviti wa serikali za mitaa kwasababu ndio viongozi wa karibu na wananchi. “Hii elimu ya huduma za fedha, tunayowaletea ni mahsusi kwenu kwasababu itawasaidia kufanya maamuzi sahihi wakati wa matumizi. Lakini pia, katika kutunza na kuweka akiba. Huduma ndogo za mikopo ya fedha, mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali, mikopo ya nyumba, elimu ya ujasiriamali pamoja na huduma za bima ya afya na bima ya mali ni muhimu kufahamu ili kuwa katika mazingira salama ya ku...

Jiji la Dodoma lapewa angalizo lishe bora kwa wananchi

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Katibu Tawala Mkoa wa Singida, ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuelezwa shughuli zinazotolewa katika banda hilo kwa upande wa Divisheni ya Kilimo Mjini. Alielezwa kuwa Kilimo Mjini kinahusiana na kilimo cha kisasa kinachojikita katika mbogamboga na matunda kutokana na ufinyu wa maeneo ya mjini wanapoishi wakulima. Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Athumani Mpanda alieleza kuwa wakulima wanapaswa kutumia maeneo yao madogo waliyonayo kwaajili ya bustani kiroba. “Hizi bustani kiroba tunazitumia kupanda mbogamboga ambazo familia itatumia na hii ni kwasababu kama una kiroba cha kustawisha maua ambayo huyatumii ni vizuri kutumia kuotesha mboga mboga ambazo zitajumuisha lishe na kupendezesha mazingira yetu” alisema Mpanda. Aliongeza kuwa elimu ya bustani za majumbani imeendelea kutolewa katika taasisi nyingi za serikali pamoja na shule za msingi na sekondari. “Tumeanzisha elimu hii kwa lengo la kuhakikisha wakulima na wale ...

TARURA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI JIJINI DODOMA

Image
#Yajipanga kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu ushiriki wa vikundi vya kijamii katika matengenezo ya barabara nchini   Na. Mwandishi Wetu, DODOMA  Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni jijini Dodoma.  TARURA inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA, Catherine Sungura amesema kuwa TARURA imejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wanayoyasimamia yanayohusu ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini. Kwa mujibu wa Sungura baadhi ya maeneo hayo ni pamoja usimamizi wa matengenezo ya kawaida, matengenezo ya maeneo korofi shughuli za maabara,mazingira na jamii. "Kupitia wataalamu wetu ambao wapo katika banda letu tumejipanga pia kutoa elimu kwa wananchi na wadau wetu wengine namna wanavyoweza kus...

Fursa ya Ufugaji wa Mbwa katika Jiji la Dodoma

Image
                                                                 Na Eupilio Anthony, DODOMA Maonesho ya sherehe za wakulima nchini inazofahamika kama Nanenane, wananchi wajitokeza kujionea mifugo, bidhaa za kilimo, uvuvi na bidhaa zilizosindikwa na wajasiliamali kutokana na mazao hayo huku wakifurahishwa na ufugaji wa mbwa kisasa. Moja kati ya wafugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Mwakaleli Mwakasege aliwaeleza wananchi anavyofanya biashara hiyo. “Mimi ni mfugaji wa mbwa kwa zaidi ya miaka 10 na leo kwenye sherehe hizi za Nanenane nimefurahi sana kuona jamii inaanza kutambua thamani ya mnyama huyu. Mbwa si tu mnyama wa kufuga kwa ajili ya ulinzi ni rafiki mkubwa wa familia, mlinzi wa mali, na kwa sasa, chanzo cha kipato kwa watu wengi kama mimi” alisema Mwakasege. Aliendelea kueleza tabia za mbwa anapoishi na binadamu ku...

RC Dendego apeleka salamu za Waziri Bashe Nanenane

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego aeleza kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutekeleza vipaumbele vya kilimo ili kuongeza tija za uzalishaji, kuchangia ongezeko la ajira pamoja na ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta ya kilimo. Aliyasema hayo wakati akisoma salamu za Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa ufunguzi wa maonesho Nanenane ya wakulima, wafugaji na wavuvi uliofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma kuanzia tarehe 01 – 08 Agosti, 2025. Alisema kuwa zipo hatua zitakazosimamiwa na wizara katika kuhakikisha nchi inakua na chakula cha kutosha wakati wote. “Wizara inatazamia kuimarisha upatikanaji wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi. Pia kuimarisha maendeleo ya ushirika na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika uendelezaji wa sekta ya kilimo” alisema Dendego. Alimalizia kwa kusema kuwa wizara imeendelea kuwashauri, kuwael...

Dkt. Mpango atoa pongezi maandalizi ya Nanenane

Image
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango atoa pongezi kwa maboresho katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika maonesho ya kitaifa ya Nanenane kwa kuongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa. Alitoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya 32 ya wakulima Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dkt. Mpango alieleza kuwa serikali imefanya maboresho makubwa yanayoonekana katika sekta hizo, ikiwemo kuimarisha uhifadhi wa mazao ya wakulima, utoaji wa chanjo kwa mifugo, na utambuzi wa mifugo kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Aidha, alisisitiza dhamira ya serikali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha chakula barani Afrika kwa kuweka mkazo kwenye uzalishaji wa mazao ya kimkakati yenye thamani kubwa ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. “Viongozi wote katika ngazi mbalimbali wanapaswa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sera za kilimo na kuwahimiza w...

Maziwa ya Mama ni kinga kamili kwa Mtoto

Image
  Na. Leah Mabalwe, DODOMA Wazazi wametakiwa kuhakikisha wanawanyonyesha watoto wao maziwa ya mama kwa kipindi kinachopaswa ili kuwajengea afya bora na kusaidia ukuwaji wa akili zao, hasa katika miaka ya awali. Wito huo ulitolewa na Afisa Lishe wa Jiji la Dodoma, Alfa Fanuel wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani, yanayofanyika kuanzia tarehe 1-7 Agosti, 2025 uliofanyika katika Kituo cha Afya Ilazo, katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo ni msingi muhimu wa afya ya mtoto, na huchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuwaji wa ubongo na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. “Utafiti unaonesha kuwa watoto wanaonyonyeshwa ipasavyo huwa na uwezo mzuri wa kiakili, kuwa na kinga thabiti ya mwili, huwa na nafasi kubwa ya kuepuka utapiamlo na maradhi ya mara kwa mara” alisema Fanuel. Aidha, alihimiza jamii kuondoa mila na desturi zinazokatisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa...

Kuwahi Kliniki Wajawazito kunaokoa Maisha ya Mama na Mtoto

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Wanawake wametakiwa kuhudhulia kliniki pale watakapo gundua kuwa ni mjamzito ili kuhakikisha afya bora ya mama na mtoto tangu hatua za awali za ujauzito na kujua maendeleo ya mtoto na kuepusha magonjwa mbalimbali. Hayo aliyasema Afisa Muuguzi Msaidizi wa Kituo cha Afya Ilazo, Anita Rweyemamu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani, yanayofanyika kuanzia tarehe 1-7 Agosti, 2025. Alisema kuwa wengi wa wanawake wanaanza kuhudhuria kliniki wakiwa tayari na mimba za miezi mitatu au zaidi jambo ambalo ni hatarishi kwa afya ya mama na mtoto. “Niwakumbushe akina mama kuna magonjwa mengi ambayo ni ya kuambukiza na yasio ambukiza yanaweza yakakukumba ikiwa ni ugonjwa wa kifafa cha mimba. Hivyo, basi mama mjamzito anatakiwa aanze kliniki mapema ili aweze kupatiwa huduma muhimu kama chanjo, virutubisho na ushauri wa kiafya. Lakini pia, tunawahimiza wenza wenu kufuatilia na kushiriki kliniki, kwani jukumu la malezi na afya ya mto...

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2025 JIJINI DODOMA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa viongozi kutambua wajibu wa kuetekeleza Dira ya Taifa 2050 na mipango ya maendeleo ya sekta ya kilimo ambayo imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa kilimo hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka, ifikapo 2030 na kuendelea. Makamu wa Rais ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa maonesho na sherehe za wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) zinazofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma. Amesema viongozi ni vema kuwajibika kuwaelekeza wakulima, wafugaji na wavuvi kuweka nguvu zaidi kwenye mazao yenye thamani kubwa sokoni, kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje pamoja na kuwekeza katika miundombinu baridi ya uhifadhi na usafirishaji. Ameongeza kwamba ni vema Viongozi kuhamasisha uwekezaji mkubwa katika teknolojia za kisasa za kilimo, ikiwemo kilimo-janja, uwekezaji katika umwagiliaji, upatikanaji wa fedha na m...