Fursa ya Ufugaji wa Mbwa katika Jiji la Dodoma
Na Eupilio Anthony, DODOMA
Maonesho ya sherehe za wakulima
nchini inazofahamika kama Nanenane, wananchi wajitokeza kujionea mifugo, bidhaa
za kilimo, uvuvi na bidhaa zilizosindikwa na wajasiliamali kutokana na mazao hayo
huku wakifurahishwa na ufugaji wa mbwa kisasa.
Aliendelea kueleza tabia za
mbwa anapoishi na binadamu kuwa yapo mambo akifundishwa anaelewa. “Mbwa anaweza
kufundishwa tabia mbalimbali, anayo akili ya haraka, na ni mnyama mwenye hisia anajua
kufariji, kulinda na pia kusaidia kwenye shughuli za kila siku. Wapo wanaotumia
mbwa kusaidia watu wenye ulemavu, wengine kwenye utafutaji wa watu waliopotea,
hata kwenye kilimo na usalama wa mashamba” alieleza Mwakasege.
Kwa upande wa kiuchumi
alieleza namna ufugaji wa mbwa una faida katika kukuza kipato. “Ufugaji wa mbwa
unaweza kugeuka kuwa biashara yenye faida kubwa. Mbwa wanaofugwa vizuri kwa
kupewa chanjo, chakula bora, na mafunzo huuzwa kwa bei nzuri, na pia huduma zao
za ulinzi hugharamiwa” alieleza huku akitabasamu Mwakasege.
Aidha, alitoa rai kwa watanzania
kujishughulisha na ufugaji wa mbwa huku akichagiza kwa kutumia msemo wake
kwamba “ Tumchukulie mbwa kama sehemu ya maendeleo ya familia na uchumi wetu, ana
thamani kubwa kuliko tulivyozoea kufikiri” alisema Mwakasege.
Kwa upande mwingine, Mtaalam na Mfugaji wa Mbwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anthony Massawe alisema kuwa amekuwa mfugaji wa mbwa kwa zaidi ya miaka nane na ameona umuhimu katika maonesho ya Nanenane kuwapa wananchi elimu na umuhimu wa kufuga mbwa kwa tija. “Kwanza kabisa, watu wengi hudhani kwamba mbwa anakula chochote, hili halina kweli. Ili mbwa awe na afya njema, awe mkakamavu, mwenye kinga dhidi ya magonjwa na aweze kutimiza majukumu yake kama ulinzi au kuwa rafiki wa familia anapaswa kulishwa lishe kamili yenye virutubisho vyote muhimu. Mbwa anahitaji mlo wenye protini kama nyama au dagaa, wanga kama wali, viazi au dona, mboga kwa ajili ya vitamini, pamoja na maji safi ya kutosha kila siku. Mbwa pia hapaswi kufungiwa bila nafasi ya kutembea au kufanya mazoezi. Anahitaji mazingira safi, yenye nafasi ya kutosha na mahali pa kujisitiri wakati wa mvua au jua kali” alisema Massawe.
Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa serikali na waandaaji wa maonesho ya Nanenane. “Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa waandaaji wa maonesho haya ya Nanenane, kwa kunipa nafasi ya kuweka banda la mbwa. Sherehe hizi zimekuwa jukwaa muhimu sana la kuelimisha, kuhamasisha na kuunganisha wafugaji, wakulima na wataalamu kutoka kila pembe ya nchi yetu pia tunapata fursa ya kushiriki na kuchangia elimu kuhusu ufugaji” alisema Massawe.
MWISHO
Imehaririwa na Nancy Kivuyo
Comments
Post a Comment