TARURA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI JIJINI DODOMA
#Yajipanga kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu ushiriki wa vikundi vya kijamii katika matengenezo ya barabara nchini
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
Wakala ya Barabara za Vijijini na
Mijini (TARURA) inashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika katika
Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni jijini Dodoma.
TARURA inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano wa TARURA, Catherine Sungura amesema kuwa TARURA imejipanga kutoa
elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wanayoyasimamia yanayohusu ujenzi
wa miundombinu ya barabara nchini.
Kwa mujibu wa Sungura baadhi ya
maeneo hayo ni pamoja usimamizi wa matengenezo ya kawaida, matengenezo ya
maeneo korofi shughuli za maabara,mazingira na jamii.
"Kupitia wataalamu wetu ambao
wapo katika banda letu tumejipanga pia kutoa elimu kwa wananchi na wadau
wetu wengine namna wanavyoweza kushirikiana na TARURA kuwezesha matengenezo
madogo madogo ya barabara kupitia vikundi vya kijamii" amefafanua Sungura.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi
kutembelea Banda la TARURA na mabanda mengine ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
ambayo yanapatikana katika hema linalosomeka "Government Zone Pavilion
2" ili wapate elimu na ufahamu kuhusu taasisi hizo.
Comments
Post a Comment