Posts

Elimu ni haki ya watoto wenye mahitaji maalum Kata ya Ipagala

Image
Na. Coletha Charles, IPAGALA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea na jitihada ya utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum kiafya kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 katika Kata ya Ipagala. Akizungumza wakati zoezi hilo, Afisa Elimu wa Kata ya Ipagala, Veronica Mpanda, aliwaomba wazazi kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalum shule kwa sababu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine kulingana na sera ya elimu jumuishi kwa kuwa miundombinu imara ipo kwa ajili yao. Alisema kuwa zoezi hilo linalenga kutambua idadi na aina ya mahitaji ya watoto hao ili kuweka mipango madhubuti ya kuwahudumia. “Zoezi hili la uandikishaji lilitakiwa lifanyike katika Shule ya Msingi ya Ipagala B, lakini hatujafanikiwa kupata mtoto hata mmoja mwenye mahitaji maalum japo zoezi hili ni endelevu na tunatambua kwamba elimu ni haki ya kila mtoto na kupitia zoezi hili tutahakikisha kuwa hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa sababu ya changamoto yoyote” alisema Mpanda. ...

Kata ya Mkonze yabainisha watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu

Image
Na. Coletha Charles, MKONZE Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea na zoezi la kubainisha watoto wenye mahitaji maalum kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka 2025, kwa ushirikiano na viongozi wa kata, mitaa na wazazi. Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkonze, Herieth Reuben, alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum kupata fursa za kielimu na kijamii zinazolingana na mahitaji yao. Alisema kuwa kata hiyo ina wakazi 41,000, mitaa nane na shule 12 za msingi. Hivyo, wamejipanga kusimamia shughuli ya uandikishaji kwa asilimia 100 na watapita kila kaya kuwabainisha watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kuanza masomo yao. “Hii ni sehemu ya mpango wetu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata haki zao za msingi bila ubaguzi, tunaomba wazazi watupe ushirikiano ili tuweze kuboresha maswala ya elimu. Lakini pia watoto wengi wenye mahitaji maalum watapata huduma stahiki, watajiunga na elimu ya msingi kwa sababu kata...

SHIKUHA kutatua kero za Abiria

Image
Na. Coletha Charles, Dodoma Katibu Mkuu wa Shirika la Kutetea Haki za Abiria nchini (SHIKUHA), Mhandisi Hashim Ramadhani, amewataka abiria kuelewa elimu na haki zao wanapotumia huduma za usafiri kwa kushirikiana na Afisa Usalama barabarani ili kuhakikisha mabasi yanazingatia sheria na huduma bora.   Akizungumza katika mkutano na wajumbe wa shirika hilo kutoka mikoa mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Rafiki Hoteli jijini Dodoma, Katibu Mkuu alifafanua kampeni za elimu zimekuwa muhimu katika kuhakikisha abiria wanakuwa na uelewa wa kina kuhusu haki zao. Alisema kuwa, elimu hiyo inatolewa kupitia stendi za mabasi, masoko na sehemu zenye mikusanyiko. Pia alibainisha kuwa maafisa wa shirika hilo watashirikiana na wadau wa sekta ya usafiri kuhakikisha sheria na kanuni zinatekelezwa kwa maslahi ya abiria. “Tumeweka msisitizo katika kuwaelimisha abiria juu ya jinsi ya kuripoti changamoto wanazokumbana nazo, kama vile kucheleweshwa kwa safari, kupotea kwa mizigo, au huduma zisi...

SHIKUHA yatakiwa kutoa elimu ya haki za Abiria

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Shirika la Kutetea Haki za Abiria (SHIKUHA) latakiwa kuwapa elimu ya kutosha abiria kwa lengo la kutatua changamoto za usalama barabarani na kufanya abiria wajuwe haki na wajibu wao. Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Rafiki Hoteli Dodoma alipomuwakilisha Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini. Prof. Mwamfupe alisema kuwa elimu itolewe wakati safari inapoanza ili abiria akipata sehemu ya kujitetea wanakuwa na amani na dereva akienda tofauti na sheria za barabarani waweze kutoa taarifa kuhusu tukio hilo kwa watu sahihi. “Rai yangu kubwa kama kuna kitu ambacho ningewahasa nyie kama shirika kulifanya hili basi ni kuwa na mpango mkakati na huo mpango utaonesha dira yenu kama mlivyosema kwenye risala na lakini mnataka kufikia wapi mwaka huu na je, tunapimaje viongozi maana nyie ni viongozi wa kitaifa kwa kutunza na kusaidia abiria” alisema Prof. Mwamfupe. Mwenyekiti wa Taifa SHIKUHA, ...

DC Shekimweri ahimiza mpango wa lishe bora shuleni

Image
Na. Aisha Ibrahim, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri aliwataka wakuu wa shule na walimu wakuu kutekeleza mpango wa huduma ya chakula kwa wanafunzi wote shuleni ili kuhakikisha wanapata lishe bora jambo litakalopelekea kujifunza kwa ufanisi. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri  Aliyasema hayo ofisini kwake wakati akihamasisha wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuandikisha watoto shuleni katika ngazi ya awali na msingi pia wale wanaojiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2025. Akisisitiza kuhusu mpango wa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni, “……kuna uhusiano mkubwa sana kati ya ufaulu na lishe, mtoto ambaye hajashiba ni ngumu sana kumsikiliza mwalimu akamuelewa na akazingatia, ni tofauti na mtoto aliyepata chakula shuleni” alisema Alhaj Shekimweri. Kwa upande wa wazazi na walezi katika Jiji la Dodoma walisema kuwa wamepokea vizuri mpango wa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni ili kuhakikisha wanapata lishe bora ikiwa ni c...

Wafanyabiashara kuboresha huduma na kukuza biashara Mwaka 2025

Na. Halima Majid na Shahanazi Subeti, DODOMA Wafanyabiashara waweka wazi malengo ya kuboresha huduma ya kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi ya Jiji la Dodoma mwaka 2025. Hayo yalisemwa na wafanyabiashara wa eneo la One Way lililopo katikati ya Jiji la Dodoma wakati wa mahojiano na waandishi wa habari walipokuwa wanaelezea salamu za jinsi walivyoupokea mwaka mpya 2025. Mfanyabiashara wa urembo, Luqman Olomi, katika Mtaa wa One Way alisema changamoto kubwa ni matatizo ya kifamilia yanayopelekea kurudishwa nyuma kiuchumi na kusababisha biashara yake kuyumba kwa kiasi flani. "Kuna changamoto za kifamilia zaidi ambazo huwa zinaturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa kwa sababu inabidi utumie mpaka kiasi ambacho umeweka kwa ajili ya biashara na ili tufanikiwe inatakiwa tujitegemee na tusitegemee cha mtu. Hiyo ndio siri ya mafanikio na kwa anayoyafanya Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na mashirika mengi na taasisi mbalimbali anafanya vizuri” alis...

Viongozi Jukwaa la Wanawake Jiji la Dodoma wawezeshwa mafunzo

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Viongozi wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamewezeshwa mafunzo ya fursa za kiuchumi katika shughuli za biashara, kilimo, upatikanaji wa mitaji, sheria, ujasiriamali, matumizi ya teknolojia na mikopo ya asilimia kumi.   Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la kuwakutanisha wananawake ili waweze kujadili fursa na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi.   Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hidaya Mizega, aliwataka wanajukwaa hao kufahamu majukumu yao na sheria katika kuwezesha mafunzo kwa wanawake wengi kwa kufahamu masuala ya uchumi.   Alisema kuwa, viongozi hao wanajukumu katika mitaa na kata zao kuhamasisha shughuli za kiuchumi kwa kuibua miradi mikubwa na mizuri kupitia mikopo ya asilimia kumi ili kukuza ongezeko la uchumi kwa wanawake, kwa kufuata mwongozo mpya ambao um...

Wazazi washauriwa kununua vifaa vya shule kwa bei elekezi

Na. Aisha Ibrahim, DODOMA                                                                                                                                                                      ...

Usafi mwisho wa Mwezi waendelea Kata ya Mnadani

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Wananchi wa Kata ya Mnadani Halmashauri ya Jiji la Dodoma walifanya usafi wa mazingira mita tano kuzunguka maeneo yao ya makazi na biashara ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la usafi, Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Usimamizi wa Taka ngumu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro, alisema kuwa ni wajibu wa viongozi kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kufanya kazi kwa pamoja na wananchi. Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na utupaji wa taka ovyo katika maeneo na kufanya usafi katika mitaro ambayo inapitisha maji machafu kipindi hiki cha mvua nyingi na kujiepusha na mafuriko yatokanayo na uzibaji wa mitaro. “Usafi ni ustaarabu ambao unaanza na mimi na wewe. Lakini katika kipindi hiki cha masika, kumekuwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali ya kuhara na kutapika ambayo tunaweza kujiepusha kwa kufanya usafi kwenye maeneo yetu” alisema Kimaro...

Madiwani wadaiwa uthubutu kufanya maamuzi ya kimaendeleo

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, wametakiwa kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi ya kimaendeleo ili kuwanufaisha wananchi wanaowasimamia. Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, alipokuwa akiwakaribisha madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mstahiki Meya, Prof. Davis Mwamfupe akifafanua jambo “Kikubwa katika mtakachokiona, sio utajiri wetu wa pesa ni uthubutu wa kufanya maamuzi, unaweza kuwa na pesa lakini hauna uthubutu wa kuzitumia, ukipewa shilingi milioni moja, utapata wasiwasi kuzitumia kwasababu zitaisha, hutakubali matumizi ya laki mbili au tatu. Lakini sisi hatuogopi, kama tuna mradi wa hoteli iliyopo hapa ambayo imegharimu shilingi Bilioni 12, hatuogopi mradi wa Soko la wazi la Machinga, ingawa serikali ilituchangia shilingi Bilioni tatu, na sisi tukaweka shilingi bilioni sita nyingine. Hatuogopi kwamb...