Wazazi washauriwa kununua vifaa vya shule kwa bei elekezi
Na. Aisha Ibrahim, DODOMA Wafanyabiashara wanaojihusisha na kuuza vifaa vya shule kwa wanafunzi, wanaopatikana Mtaa wa One Way, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wamewaasa wazazi na walezi kujitokeza kununua vifaa hivyo kwa bei elekezi bila kuhofia, kwasababu mpaka sasa bei ni ya kawaida kama ilivyokuwa miezi iliyopita .
Hayo yalisemwa na baadhi ya wafanyabiashara
wakieleza kuwa, bei ya vifaa vya shule kwa wanafunzi haijapanda kama
walivyozoea misimu iliyopita hivyo, wazazi au walezi wajitokeze kwa wingi
kununua vifaa vya shule kwa ajili ya watoto wao.
Noely Chibarabara alisema “bei zetu kwakweli
hazijapanda, ziko palepale na hakuna shida yoyote ambayo imeweza kutokea kwamba
tumepandisha bei, bei ipo palepale na bei zetu ni nzuri".
Akizungumzia kuhusu changamoto ya uzalishaji
bidhaa viwandani kutokana na uhitaji mkubwa wa wateja, mfanyabiashara Paskali
Faustine alisema bei inapanda msimu huu kutokana na uhitaji mkubwa wa bidhaa
zitumikazo shuleni.
“Bei inapanda miezi hii kwa sababu ya
uzalishaji viwandani unakuta ni changamoto, wanaotaka mahitaji ni wengi sana
kwa sababu ni kipindi cha shule asilimia kubwa bidhaa zinakuwa ziko juu”
alisema Faustine.
Akiongelea wafanyabiashara wanaopandisha bei katika
msimu wa kuelekea shule kufunguliwa, mfanyabiashara Tonni Jamen aliwashauri kutokupandisha
bei vifaa vya shule. Aidha, aliwashauri kuuza vifaa hivyo kwa bei elekezi ili
kuwawezesha wazazi na walezi kumudu gharama na kuwashauri wasiogope kujitokeza
kuwanunulia vifaa vya shule watoto wao ili waweze kwenda shule bila vikwazo.
MWISHO
Comments
Post a Comment