Posts

Jiji la Dodoma kuanza ujenzi wa Jengo Jumuishi Kituo cha Afya Makole

Image
Na. Faraja Mbise, MAKOLE Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatarajia kuanza ujenzi wa Jengo Jumuishi katika Kituo cha Afya Makole ambao unatarajiwa kuanza tarehe 27 Januari, 2025 chini ya Mkandarasi Mohanmmedi Builders Limited. Akizungumzia kuhusu huduma zitakazokuwa zinapatikana katika jengo hilo jumuishi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole, Dkt. Revocatus Baltazary alisema zitapatikana huduma mbalimbali kwa ajili ya kukidhi huduma zote za kiafya. “Jengo hili linaenda kujibu yote hayo, kwasababu huduma zitakazoenda kupatikana ni huduma za ‘emergency’, radiolojia, maabara, vyumba vya madaktari vitaongezwa. Pia kuna wodi za kulaza watoto chini ya umri wa miaka mitano, magonjwa ya ndani kwa wanawake na wanaume. Vilevile, wodi za upasuaji na ‘floor’ ya wakina mama wajawazito” alisema Dkt. Baltazary. Sambamba na hilo, alisema kuwa lengo hasa la kujenga jengo hilo ni kukosekana kwa baadhi ya huduma kama ‘emergency’, huduma za kulaza, na jengo la upasua. “Jengo hili linajengwa kutoka...

Matukio katika Picha Mafunzo ya NeST kwa Wakuu wa Shule ya Sekondari Jiji la Dodoma

Image
 

Wakuu wa Shule Jiji la Dodoma wapewa mafunzo ya mfumo wa NeST

Image
  Na. Coletha Charles, DODOMA Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamewezeshwa mafunzo ya ununuzi kwa njia ya mtandao serikalini ‘ National e-Procurement System of Tanzania’ (NeST) yatakayoboresha utendaji kazi na kuwawezesha kupata mafundi na watoa huduma kupitia mfumo wa manunuzi. Mafunzo hayo yalitolewa na Kitengo cha Manunuzi na Ugavi kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwazi kwa kufanya shughuli za ununuzi kutokana na mabadiliko ya Sheria ya Mwaka 2023 na Kanuni za Manunuzi za Mwaka 2024, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Afisa Elimu Vifaa na Takwimu, Fredrick Mwakisambwe, alifafanua mfumo wa manunuzi kwa njia ya kielektroniki, ni mfumo ambao unarahisisha mchakato wa manunuzi na kuleta ufanisi mkubwa katika utendaji kazi. Alisema kuwa mafunzo hayo ni mahususi kwa wakuu wa shule wakiambatana na walimu wanaohusika kuratibu na kusimamia fedha ambazo zinapelekwa katika shule za sekondari kw...

Ziara ya Kamati ya Fedha na Utawala katika Kituo cha Afya Zuzu

Image
  Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma (route 2) Naibu Meya, Fadhili Chibago ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa ukamilishaji wa maabara tatu katika Shule ya Sekondari Zuzu iliyopo Kata ya Zuzu.   Mradi huo unagharama ya shilingi 85,000,000.00 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji.   Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma (route 2) Naibu Meya, Fadhili Chibago ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa ukamilishaji wa maabara tatu katika Shule ya Sekondari Zuzu iliyopo Kata ya Zuzu.   Mradi huo unagharama ya shilingi 85,000,000.00 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji.  

Ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu wafikia 98%

Image
Na. Dennis Gondwe, ZUZU UJENZI wa Kituo cha Afya Zuzu umefikia asilimia 98 ya utekelezaji kikitarajiwa kuhudumia wananchi 10,054 kwa kuwahakikishia huduma bora za afya na kuwaondolea hadha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya. Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Goodluck Magoti alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu kwa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Magoti alisema “kutokana na changamoto ya kukosa huduma za Kituo cha Afya katika Kata ya Zuzu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilianza ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu ili kusogeza huduma za matibabu mbalimbali karibu na wananchi. Halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi 299,439,348,54. Hadi kufikia sasa kiasi cha shilingi 285,4439,000,54 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara na kubakiwa na shilingi 14,000,348.54 kwa ajil...

DC Shekimweri ahimiza usafi kudhibiti magonjwa Dodoma

Image
  Na. Shahanazi Subeti, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri aliitaka jamii kuzingatia suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kujikinga na magonjwa na kufanya mji kuwa safi na salama katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti ya halmashauri ili wananchi wawe na afya bora. Aliyasema hayo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupokea na kujadili mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2025/2026. Alhaji Shekimweri alisema “ wenzetu maafisa afya, watendaji wa kata, changamoto za uchafu wa mji wetu ni usimamizi kwa sehemu fulani, yapo maeneo ya kampuni za usafi, yapo maeneo yanavikundi vya usafi, lakini ni wajibu wa mwananchi mmoja mmoja kufanya usafi wa eneo lake. Kwahiyo, tuimarishe usimamizi, na kuna makampuni na vikundi na vinalipwa kwa kufanya kazi hizo ” . Akiongelea suala la usalama katika Halmashauri y...

Dodoma Jiji U-20 yakita Kambi Kileleni

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA Klabu ya soka ya Dodoma Jiji chini ya umri wa miaka 20 (U-20) imeendeleza ubabe kwa wapinzani wake wanaoshiriki ligi ya vijana ya NBC chini ya umri wa miaka 20 Tanzania bara baada ya kuwashushia kichapo cha mabao 2-1 wanajeshi wa mpakani Mashujaa FC U-20, katika mchezo uliovulumishwa katika nyasi za dimba la Jamhuri Dodoma hapo jana. Baada ya mchezo kutamatika kocha wa Dodoma Jiji U-20, Jeremiah Chido alisema “ mchezo umemalizika salama na tumepata kitu ambacho tulikua tunakihitaji ambacho ni alama tatu muhimu. Alama ambazo zinatufanya tuendelee kuwa kileleni katika kundi letu na kutufanya tusicheze kwa presha michezo inayokuja mbele yetu, michezo ambayo tutakuwa ugenini ”. Katika hatua nyingine Chido akaweka wazi malengo yao kwenye msimu huu wa Ligi ya Vijana ya NBC Tanzania Bara. “ Malengo yetu msimu huu ni kuchukua ubingwa kwasababu msimu uliopita tulifika fainali ila bahati haikuwa upande wetu. Kwahiyo, msimu huu tukishirikiana halmashauli, mashabiki...

Prof. Mwamfupe; Taka ni fursa ya kutengenezea mbolea

Image
  Na. Aisha Haji, DODOMA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na kutumia takataka zinazotokana na mazao kama fursa ya kutengeneza mbolea ili kuweza kuinua sekta ya kilimo na uchumi wa halmashauri kiujumla. Aliyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa majadiliano na Kamati ya Ushauri ya Wilaya iliyokutana kupitia mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Akizungumza kuhusu umuhimu wa mbolea zitokanazo na takataka za mazao, alisema kuwa taka za mazao ambazo zinaoza kwa urahisi ni fursa nzuri sana ya kiuchumi kuweza kutengeneza mbolea. Pia alidokeza kuwa halmashauri imejipanga katika suala la kutoa mikopo, mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa wananchi kuhusu namna ya kutumia taka zitokanazo na mazao kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku kwa kufuata utaratibu maalumu. Prof. Mwamfupe alisema “halmashauri itak...

Mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa NeST kwa Walimu Wakuu Jiji la Dodoma

Image