Kata ya Mnadani watakiwa kuandikisha watoto Darasa la Kwanza
Na. Dennis Gondwe, MNADANI JAMII imetakiwa kuhakikisha watoto wenye umri wa kuandikishwa shule za msingi wanaandikishwa kwa wakati waweze kupata elimu kwa mujibu wa sheria. Wanafunzi wakiwa darasani (picha kutoka maktaba) Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Elimu Kata ya Mnadani, Robert Tesha alipokuwa akiongea kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika Kata ya Mnadani jijini Dodoma. Tesha alisema “zoezi la uandikishaji kwa shule za msingi limeanza tangu mwezi Oktoba mwaka huu. Watoto wanaoandikishwa ni darasa la awali kuanzia miaka minne hadi mitano na darasa la kwanza miaka sita hadi nane na uandikishaji hauna gharama yoyote. Mzazi unapokwenda unatakiwa kwenda na cheti cha mtoto cha kuzaliwa na kama hauna unapitia kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa anakuandikia barua na majina kamili ya mwanafunzi kwa sababu majina yanaingizwa kwenye mfumo na hilo jina halitabadilika mpaka chuo kikuu. Niombe sana waleteni watoto tuwaandikishe shule, madarasa yameshajengwa na mama...