Posts

RAIS, DKT SAMIA ATOA BIL 4.5 KULIPA FIDIA WANANCHI DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi 469 wa maeneo mbalimbali katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kayombo alisema “Mheshimiwa Rais kwa upendo wake ameleta fedha shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Jumla ya wananchi 469 wanatarajia kulipwa kuanzia sasa, fedha tumezipokea tayari”. Akiongelea changamoto ya ‘double allocation’, alisema kuwa Rais alielekeza wananchi hao wa...

SERIKALI YATOA BIL 1 UJENZI HOSPITALI YA WILAYA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA SERIKALI imetoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma kwa lengo la kuboresha huduma za afya na kuzisogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo akiongea na waandishi wa habari Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kayombo alisema “kwa upande wa afya mheshimiwa rais ameleta fedha nyingi. Ameleta shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma inayojengwa eneo la Nala. Kituo cha Afya Makole kimekuwa kikipokea watu wengi sana, mheshimiwa Rais ametuletea shilingi milioni 750 kwa ajili...

JIJI LA DODOMA LAPOKEA ZAIDI YA BIL 5 SEKTA YA ELIMU MSINGI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepokea zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya elimu ya msingi kutoka kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kayombo alisema “kwa upande wa elimu ya msingi, tumepokea zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya elimu ya msingi. Tumepokea shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya tatu ambazo ujenzi unaendelea”. Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknol...

RAIS DKT. SAMIA ATOA FEDHA KIBAO KUTEKELEZA MIRADI JIJI LA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuboresha maisha ya watanzania. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo akiongea na waandishi wa habari Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kayombo alisema “Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika sekta ya elimu sekondari. Mheshimiwa Rais ametuletea shilingi 260,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari ya wasich...

KLINIKI YA ARDHI JIJI LA DODOMA YAHUDUMIA WANANCHI 3,056 NDANI YA SIKU 5

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA KLINIKI ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imehudumia wananchi 3,056 waliokuwa na kero za muda mrefu kuhusiana na sekta ya Ardhi yakiwa ni mafanikio makubwa kwa   wananchi wengi kuhudumiwa kwa muda mfupi. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo Takwimu hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake. Kayombo alisema “zoezi hili limetoa matokeo chanya kwa ujumla. Wananchi 3,056 walisikilizwa. Hati 1,474 zilitolewa papo hapo. Maombi mapya ya hati 561 yalipokelewa, namba za malipo 1,674 zilitolewa, viwanja 645 vilipandishwa kwenye mfumo, migogoro ya ardhi 774 ilisikilizwa, wananchi 149 walipata huduma za Mipango Miji na wananchi 221 walipata huduma za upimaji” alisema Kayombo. Akiongelea kliniki hiyo, alisema kuwa ililenga kutatua changamoto za Ardhi kwa haraka. “Zoezi hili ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa mkakati wa Mkoa wa Dodoma wa kumaliza changamoto za Ard...

WIZARA YA ARDHI KUBORESHA MFUMO WA ILMIS

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kuboresha mfumo wa kieletroniki wa kutunza taarifa za Ardhi (ILMIS) ili kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa hati milki ikiwa niutekelezaji maelekezo ya serikali. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa akiongea na waandishi wa habari Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dodoma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Slaa alisema “tarehe 3 Oktoba, 2023 serikali ilitoa maelekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Maelekezo hayo yalihusu mamlaka mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa sekta ya Ardhi. Wizara inaendelea na uboreshaji wa mfumo wa kieletroniki wa kutunza t...

JIJI LA DODOMA LAPEWA HADHI YA MKOA WA ARDHI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yaipa Halmashauri ya Jiji la Dodoma hadhi ya kuwa Mkoa wa Ardhi kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dodoma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Slaa alisema “Wizara imeifanya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa Mkoa wa Ardhi kiutendaji ikiwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi ambae atahudumia eneo hilo na halmashauri nyingine kuwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mwingine”. Waziri huyo alisema kuwa wizara imeandaa utaratibu wa kutoa huduma kwa pamoja katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma utaratibu ambao utasimamiwa na wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuanzia tarehe 30 Oktoba,...

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA TATU YA KLINIKI YA ARDHI DODOMA

Image
 

WANANCHI WAASWA KUIBUA MALALAMIKO YA ARDHI YALIYOFUNGWA JIJI LA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuacha tabia ya kufanya bahati nasibu ya kupata haki isiyostahili baada ya kuwa malalamiko yao yamekwisha tatuliwa kwa mujibu wa taratibu na sheria. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiongea na wananchi waliojitokeza kupata huduma ya Ardhi katika Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kutatuliwa kero na malalamiko yao kwenye Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika siku yake ya tatu jijini hapa. Senyamule alisema “nisisitize tunaposhughulikia kero hizi niombe wananchi wa Dodoma na kutoa wito najua kuna watu wanajirudiarudia kila wakati ambao kero zao zilishafungwa ila wanajaribu bahati nasibu nyingine. Nitoe rai wale ambao kero zao zilishafungwa huna haja ya kutumia masaa yako hapa, utapata jibu lilelile ambalo ulishalipata. Tukimaliza tatizo lako tunalifunga na tunapeana taarifa, naka...

DODOMA ISIYO NA KERO ZA ARDHI YATAJWA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu yasiyokuwa na kero wala migogoro ya Ardhi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (kushoto) akikabidhi moja ya Hati zilizotolewa siku a tatu ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kuhudumiwa na kutatuliwa kero zao katika Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya tatu jijini Dodoma. Senyamule alisema “niwahakikishie Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama mwenye upendo na mama anayewapenda watanzania, jambo hili halitaki na anatamani wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu ya Dodoma na watafurahia kama watapa haki zao. Ndiyo maana amekuwa akituagiza kutatua kero zao hasa za Ardhi katika Jiji la Dodoma. Kama mkoa baada ya kupokea maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wametuagi...