DODOMA ISIYO NA KERO ZA ARDHI YATAJWA
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wa Dodoma
wafurahie makao makuu yasiyokuwa na kero wala migogoro ya Ardhi.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (kushoto) akikabidhi moja ya Hati zilizotolewa siku a tatu ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma |
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary
Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kuhudumiwa na
kutatuliwa kero zao katika Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya tatu
jijini Dodoma.
Senyamule alisema “niwahakikishie Mheshimiwa Rais,
Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama mwenye upendo na mama anayewapenda watanzania, jambo
hili halitaki na anatamani wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu ya Dodoma na
watafurahia kama watapa haki zao. Ndiyo maana amekuwa akituagiza kutatua kero
zao hasa za Ardhi katika Jiji la Dodoma. Kama mkoa baada ya kupokea maelekezo ya
Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi wametuagiza kuhakikisha tunamaliza kero za Ardhi kwa wananchi wa Dodoma”.
Alisema kuwa mkoa umetengeneza mpango mkakati wa mwaka
mmoja kuhakikisha kero za Dodoma zinaisha. “Kuanzia mwezi Julai hadi Desemba,
2023 kuna kero kubwa zinazogusa makundi makubwa tunaendelea kuzitatua. Kuanzia mwezi
Januari hadi Juni, 2024 tunamalizia kero za mtu mmoja mmoja ambazo
hazikukamilika kwa wakati. Nimpongeze Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mkurugenzi wa
Jiji na Katibu Tawala Mkoa baada ya mkakati huu wameendelea kuunyumbulisha ili
ukamilike vizuru wameongeza na ubunifu. Mfano kuanzisha hii Kliniki ya Ardhi ni
moja ya mkakati wa kukamilisha kero kwa wakati” alisema Senyamule.
MWISHO
Comments
Post a Comment