JIJI LA DODOMA LAPOKEA ZAIDI YA BIL 5 SEKTA YA ELIMU MSINGI
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepokea zaidi ya
shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya elimu ya msingi kutoka
kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.
Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo |
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi
wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na
Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Kayombo alisema “kwa upande wa elimu ya msingi,
tumepokea zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya
elimu ya msingi. Tumepokea shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule
mpya tatu ambazo ujenzi unaendelea”.
Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano
na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa program hiyo ni muhimu
kuzungumzia maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini. “Serikali ya Rais, Dkt.
Samia Suluhu Hassan imekusikia imekufikia, wale wafanyakazi waliokaa miaka
kadhaa mshahara haujapanda tumekusikia tumekufikia, wale waliokuwa wanateseka
na maji safi na salama hayapo, tumekusikia tumekufikia, wale ambao ilikuwa ni
lazima kumsafirisha mgonjwa wake kumpeleka Dar es Salaam kwenda kutibiwa tumekusikia
tumekufikia, ni kampeni rahisi na inaeleka” alisema Waziri Nnauye.
MWISHO
Comments
Post a Comment