JIJI LA DODOMA LAPEWA HADHI YA MKOA WA ARDHI
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WIZARA
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yaipa Halmashauri ya Jiji la Dodoma
hadhi ya kuwa Mkoa wa Ardhi kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.
![]() |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa |
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika Ofisi ya Ardhi Mkoa wa
Dodoma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu kuboresha huduma za
sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza.
Slaa
alisema “Wizara imeifanya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa Mkoa wa Ardhi
kiutendaji ikiwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi ambae atahudumia eneo hilo na
halmashauri nyingine kuwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mwingine”.
Waziri
huyo alisema kuwa wizara imeandaa utaratibu wa kutoa huduma kwa pamoja katika Halmashauri
ya Jiji la Dodoma utaratibu ambao utasimamiwa na wizara kwa kushirikiana na Halmashauri
ya Jiji la Dodoma kuanzia tarehe 30 Oktoba, 2023. “Hatua hizi zinalenga
kuboresha utoaji wa huduma za sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma. Nitoe wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo kupata huduma za sekta ya Ardhi
zikiwemo upatikanaji wa hati milki, malipo ya kodi ya pango la Ardhi, utatuzi
wa migogoro na utoaji wa elimu kwa wananchi” alisema Slaa.
Comments
Post a Comment