Posts

KAMATI YA LAAC YARIDHISHWA MRADI WA KITEGA UCHUMI WA BIL. 18 JIJI LA DODOMA

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeridhishwa na ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi Mtumba kwa shilingi bilioni 18 lililojengwa kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani ya Halmshauri ya Jiji la Dodoma. Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Stanslaus Mabula Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Stanslaus Mabula baada ya kupokea taarifa ya Jengo la Kitega Uchumi Mtumba la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa kisasa wa mikutano wa halmashauri hiyo. Mabula alisema “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, tumesikiliza taarifa zote tatu. Kwanza niwapongeze sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufikiria kuwa na vitega uchumi ambavyo kiukweli vitaipaisha halimashauri hii. Sisi kama Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, tumekuwa na msisitizo kila wakati kwanza kuhakikisha halmashauri nchini zinaongeza mapato yake. Pili, zibuni vyanzo vingi zaidi ili ziweze kuon...

RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATAKA KULINDA MAADILI YA JAMII

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amelitaka Kanisa la Anglikana kulinda maadili na kukemea maovu kwa vijana ili wawe raia wema katika jamii. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu jijini Dodoma  Kauli hiyo aiitoa alipokuwa mgeni rasmi katika tukio la ufunguzi wa jengo la kitega uchumi (Safina house) la Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, tukio lililofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu jijini hapa. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema “nihimize kulinda maadili na kukemea maovu katika jamii kwa vijana. Lakini wapo wakubwa wanaolitumia kanisa kufanya maovu, kemeaneni”. Aidha, Rais alilipongeza kanisa ...

TAKUKURU YAIBUKA NA PROGRAM YA USHIRIKI WANANCHI KUKABILI VITENDO VYA RUSHWA

Image
Na Tabitha Joshua, CHANG’OMBE Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imeanzisha programu iitwayo TAKUKURU Rafiki inayolenga kuongeza ushiriki wa wananchi katika kukabili vitendo vya rushwa kwa jamii. Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Michael Sanga Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Michael Sanga katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Chang’ombe iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Sanga alisema “TAKUKURU Rafiki ipo kwa lengo la kufikia wananchi kwa karibu na kutatua kero zao wenyewe ambazo zinapatikana katika idara zote, zinazopatikana katika kata hii. Vikao vyote vinavyohusu TAKUKURU Rafiki vinafanywa katika ngazi ya kata Mwenyekiti wake ni diwani wa kata na katibu wake anakuwa ni Afisa Mtendaji wa Kata”. Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe, Tunu Dachi aliishukuru Ofisi ya TAKUKURU kwa kuanzisha proramu hii kwasababu imeweza kuondoa kero za wananchi katika kata...

ASMA KARAMA ACHAGULIWA NAIBU MEYA JIJI LA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA ASMA Said Karama amechaguliwa kwa asilimia 100 kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri. Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Said Karama Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Naibu Meya, Sakina Mbugi alisema “Mheshimiwa Asma Said Karama amepata kura 55 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa na wajumbe. Kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza Mheshimiwa Asma Said Karama kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma”. Akitoa neno la shukrani Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Karama alisema alimshukuru Mungu kwa baraka zake. “Napenda kukishukuru chama changu cha Mapinduzi kwa kuniruhusu kuingia kinyang’anyiro hiki. Kipekee zaidi napenda kuwashukuru madiwani kwa kuniamini na kunituma ili niwatumikie, tufanye kazi pamoja na kumsaidia Mstahiki Meya na kuwaletea maendeleo wana Dodoma. Kipekee zaidi nashukuru ...

MEYA AKEMEA UZALISHAJI MIGOGO JIJI LA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amekemea tabia ya uzalishaji migogoro ya ardhi na kusema inarudisha nyuma maendeleo ya halmashauri. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe Prof. Mwamfupe alisema hayo alipokuwa akitoa muhtasari wa hoja zilizoibuliwa katika Mkutano wa Chama wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema “tunakemea watu wote wanaojihusisha na kuzalisha migogoro katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Na katika hili Mkurugenzi wa Jiji, watumishi wachukue nafasi zao na kwamba tutasimama kuhakikisha hatuibui migogoro mingine ya ardhi. Yapo maeneo madiwani wake wametuhumiwa kuhusika na migogoro ya ardhi. Rai ya kikao ilikuwa hawa wajitokeze tufanye nao mkutano wa Pamoja Meya, Mkurugenzi wa Jiji na Mkuu wa Divisheni ya Uendelezaji Makao Makuu. Mkutano huo ni wa kuwataka kutoa picha ya muelekeo wao na jinsi wanavyoifaham...

WAJUMBE WA KAMATI YA FEDHA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUJIHOJI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WAJUMBE wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuhoji utendaji kazi wa halmashauri na kutoa ushauri utakaoifanya halmshauri hiyo kusonga mbele. Mwenyekiti wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe baada ya kuunda Kamati ya Fedha na Utawala katika mkutano wa wazi uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji. Prof. Mwamfupe ambae ni Mstahiki Meya alisema kuwa Kamati ya Fedha na Utawala kwa mujibu wa kanuni itaongozwa na Mstahiki Meya. Wajumbe wake ni Mbunge Anthony Mavunde, Naibu Meya Asma Karama, Joan Mazanda, Daud Mkhandi, Jumanne Ngede, Bakari Fundikila, Ased Ndajilo, Grace Milinga, Neema Mwaluko na Elis Kitendya. “Yeyote aliyepangwa katika kamati hii atangulie kuamini kwamba ni imani yangu kwake, kwamba anaweza kufanya hivyo kuliko vinginevyo kwamba huyu alikuwa anataka hizi kamati siyo baraza...

JIJI LA DODOMA LAISHUKURU SERIKALI FEDHA ZA MAENDELEO

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jambo lililosogeza huduma za kijamii na maendeleo karibu na wananchi. Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda Shukrani hizo zilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi na uwajibikaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 katika Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo. Kaunda alisema kuwa katika mwaka wa fedha ulioisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliweza kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi. “Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma tunapenda kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awa...

KILIMO CHA ZABIBU 88 DODOMA

 

WAAJIRI DODOMA WATAKIWA KUSAIDIA WANAWAKE KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YA MAMA KAZINI

Image
Na. Dennis Gondwe Dodoma, WAAJIRI katika Mkoa wa Dodoma wametakiwa kutoa msukumo katika kurahisisha na kusaidia wanawake walioajiriwa kuendelea kunyonyesha watoto wao kwa mujibu wa taratibu ili wawe na lishe bora. Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akiongea na mamia ya wananchi  Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika hotuba yake kwenye matembezi ya hiari kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na kusomwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri yaliyoishia uwanja wa Shule ya Msingi Chang’ombe jijini hapa. Senyamule alisema kuwa lengo kuu la maadhimisho ya mwaka huu ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kusaidia wanawake waweze kufanya kazi za uzalishaji pamoja na utunzaji wa watoto wao. Alisema kuwa ili kufanikiwa “lazima kuhamasisha na kutetea utekelezaji wa mikakati inayowezesha waajiri kuwa karibu na familia, walezi au mama wa mtoto na kutoa msukumo katika kurahisisha ...

WENZA WA VIONGOZI WASHAURIWA KUANZISHA BUSTANI ZA NYUMBANI

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WENZA wa viongozi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kuanzisha bustani za nyumbani ili kusaidia familia zao na wageni wanaowatembelea. Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lucy Kway Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lucy Kway alipokuwa akiongelea umuhimu wa bustani za nyumbani kwa wenza wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alipokuwa akihamasisha kilimo cha bustani hizo kwenye Banda la Jiji la Dodoma katika viwanja vya Nanenane Nzuguni. Kway alisema “nichukue nafasi hii kuwashauri wenza wa viongozi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kulima bustani za nyumbani kwa ajili ya kusaidia familia zao na wageni wanaowatembelea. Hii ni muhimu kwa sababu wenza wa viongozi ni mfano wa kuigwa katika jamii hivyo ni rahisi kwa watu kuiga mfano mzuri kutoka kwa wenza wa viongozi hapa Halmashauri ya Jiji la Dodoma”. Akiongelea kilimo hicho kwa wananchi na watumishi wanaohamia Makao Makuu Do...