WAJUMBE WA KAMATI YA FEDHA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUJIHOJI
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WAJUMBE wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri
ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuhoji utendaji kazi wa halmashauri na kutoa
ushauri utakaoifanya halmshauri hiyo kusonga mbele.
![]() |
Mwenyekiti wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe |
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Mwaka
wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe baada ya kuunda Kamati ya Fedha na Utawala
katika mkutano wa wazi uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji.
Prof. Mwamfupe ambae ni Mstahiki Meya alisema kuwa
Kamati ya Fedha na Utawala kwa mujibu wa kanuni itaongozwa na Mstahiki Meya. Wajumbe
wake ni Mbunge Anthony Mavunde, Naibu Meya Asma Karama, Joan Mazanda, Daud
Mkhandi, Jumanne Ngede, Bakari Fundikila, Ased Ndajilo, Grace Milinga, Neema
Mwaluko na Elis Kitendya.
“Yeyote aliyepangwa katika kamati hii atangulie
kuamini kwamba ni imani yangu kwake, kwamba anaweza kufanya hivyo kuliko
vinginevyo kwamba huyu alikuwa anataka hizi kamati siyo baraza la uwakilishi
ambapo kila jimbo lazima liwe na mtu. Ndiyo maana wakati mwingine tumepewa
vipaji mbalimbali. Kwangu naongozwa na ukweli kwamba nataka tuhoji. Sisi ni
wasimamizi nataka tuwe na uwezo wa kuhoji na kushauri vizuri” alisema Prof.
Mwamfupe.
MWISHO.
Comments
Post a Comment