Posts

KILIMO CHA ZABIBU 88 DODOMA

 

WAAJIRI DODOMA WATAKIWA KUSAIDIA WANAWAKE KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YA MAMA KAZINI

Image
Na. Dennis Gondwe Dodoma, WAAJIRI katika Mkoa wa Dodoma wametakiwa kutoa msukumo katika kurahisisha na kusaidia wanawake walioajiriwa kuendelea kunyonyesha watoto wao kwa mujibu wa taratibu ili wawe na lishe bora. Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akiongea na mamia ya wananchi  Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika hotuba yake kwenye matembezi ya hiari kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na kusomwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri yaliyoishia uwanja wa Shule ya Msingi Chang’ombe jijini hapa. Senyamule alisema kuwa lengo kuu la maadhimisho ya mwaka huu ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kusaidia wanawake waweze kufanya kazi za uzalishaji pamoja na utunzaji wa watoto wao. Alisema kuwa ili kufanikiwa “lazima kuhamasisha na kutetea utekelezaji wa mikakati inayowezesha waajiri kuwa karibu na familia, walezi au mama wa mtoto na kutoa msukumo katika kurahisisha ...

WENZA WA VIONGOZI WASHAURIWA KUANZISHA BUSTANI ZA NYUMBANI

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WENZA wa viongozi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kuanzisha bustani za nyumbani ili kusaidia familia zao na wageni wanaowatembelea. Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lucy Kway Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lucy Kway alipokuwa akiongelea umuhimu wa bustani za nyumbani kwa wenza wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alipokuwa akihamasisha kilimo cha bustani hizo kwenye Banda la Jiji la Dodoma katika viwanja vya Nanenane Nzuguni. Kway alisema “nichukue nafasi hii kuwashauri wenza wa viongozi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kulima bustani za nyumbani kwa ajili ya kusaidia familia zao na wageni wanaowatembelea. Hii ni muhimu kwa sababu wenza wa viongozi ni mfano wa kuigwa katika jamii hivyo ni rahisi kwa watu kuiga mfano mzuri kutoka kwa wenza wa viongozi hapa Halmashauri ya Jiji la Dodoma”. Akiongelea kilimo hicho kwa wananchi na watumishi wanaohamia Makao Makuu Do...

CHEMS YAJIKITA KUZALISHA MADUME BORA YA MBUZI DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA CHEMS farm imedhamiria kuzalisha madume bora ya Mbuzi aina ya Boha ili kuwasaidia wafugaji kuboresha mifugo yao ya asili katika kanda ya kati. Mfugaji wa Mbuzi kutoka Chems farm, Vendelin Lyakurwa Kauli hiyo ilitolewa na Mfugaji wa Mbuzi kutoka Chems farm, Vendelin Lyakurwa alipokuwa akielezea ufugaji wa Mbuzi katika Banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini hapa. Lyakurwa alisema “lengo la kuzalisha na kuwatunza hawa Mbuzi aina ya Boha ni kuuza madume kwa wenzetu ili waweze kuboresha mifugo yao ya asili. Ukiwa na dume moja kwenye boma unaweza kukusaidia kupata mbegu ambayo wanakua haraka na bei yao ni nzuri na nyama yao ni tamu. Mbuzi hawa ni wa nyama na wanazaa mapacha ukiwalisha vizuri wanazaa pacha watatu mpaka wanne. Wanakuwa haraka wanasoko mpaka uarabuni wanawahitaji hawa Mbuzi. Ni Mbuzi ambao ‘wanaadapt’ mazingira mbalimbali”. Alisema kuwa madume wakitumika kwa Mbuzi wa ki...

JIJI LA DODOMA LAJA NA TEKNOLOJIA YA NISHATI MBADALA MAONESHO YA NANENANE

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeanzisha teknolojia ya nishati mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya kati. Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George Joram Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George Joram alipokuwa akiongelea teknolojia ya nishati mbadala inayooneshwa katika banda la mifugo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Joram alisema “safari hii tumekuja na teknolojia ya nishati mbadala. Tunazalisha gesi kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe. Kinyesi cha ng’ombe tunakikusanya kutoka kwenye banda la ng’ombe tunachanganya kwa mchanganyo wa moja kwa moja. Tunachukua kinyesi cha ng’ombe kwenye ndoo ya lita 20 na maji lita 20 tunachanganya na kuzalisha gesi”. Alisema kuwa baada ya saa 24 bacteria wanazalisha gesi inayoitwa Methane. “Badala ya kutumia mkaa na nishati nyingine kama kuni, unaweza kutumia nishati mbadala ya kutumia gesi ya kinyesi cha mifugo na kulinda na ku...

WAFUGAJI DODOMA WASHAURIWA KULIMA MALISHO

Image
Na. Dennis Gondwe, NANENANE- ZUGUNI WAFUGAJI katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufanya ufugaji wa ndani na kulima malisho ya mifugo ili kujihakikishia kipato. Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipotembelea Banda la Mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma. Mchomvu alisema “tunahimiza wafugaji kufanya ufugaji wa ndani. Hivyo, ni muhimu mfugaji alime malisho yake kwa ajili ya kujiongezea kipato na tija ya maziwa na nyama. Wakati mwingine tunawafundisha ambao siyo wafugaji kulima malisho kama zao la biashara. Dodoma upatikanaji wa majani ni mgumu hivyo, mtu anaweza kulima malisho kama zao la biashara akayakata akayaanika na kuyafunga katika mfumo wa bezi na kuwauzia wafugaji. Na soko lipo wazi kabisa kwa wafugaji na bei ni nzuri beli moja tunalipata kwa shilin...

BANDA YA JIJI LA DODOMA LATOA TEKNOLOJIA UFUGAJI SAMAKI NA KUKU PAMOJA

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamehamasishwa kujifunza teknolojia ya ufugaji wa samaki na kuku kwa pamoja ili kujiongezea kipato. Afisa Uvuvi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tausi Kiula Hamasa hiyo ilitolewa na Afisa Uvuvi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tausi Kiula alipokuwa akihamasisha ufugaji wa pamoja wa samaki na kuku kwa wananchi waliotembelea banda la mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kiula alisema “tunawahamasisha wananchi wote waje wajifunze katika bwawa letu hapa. Kama unavyoona teknolojia nzuri ya kisasa ambayo unapoiona unahamasika. Unachimba bwawa la samaki kisha unajenga kibanda cha kuku kwa juu yake ili kuku wakiwa wanajisaidia kinyesi kinadondoka katika bwawa la samaki na kusaidia ‘fertilization’ kwa kuweka mbolea inayobadilisha maji kuwa ya kijani na kutengeneza chakula cha samaki”. Akiongelea umuhimu wa ufugaji huo alisema kuwa unawahakikishia samaki chakula bora. “Maji yanapobadilika kwenda rangi ya k...

WAFUGAJI KANDA YA KATI WASHAURIWA KULIMA MALISHO YA MIFUGO

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WAFUGAJI katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufanya ufugaji wa ndani na kulima malisho ya mifugo ili kujihakikishia kipato. Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipotembelea Banda la Mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma. Mchomvu alisema “tunahimiza wafugaji kufanya ufugaji wa ndani. Hivyo, ni muhimu mfugaji alime malisho yake kwa ajili ya kujiongezea kipato na tija ya maziwa na nyama. Wakati mwingine tunawafundisha ambao siyo wafugaji kulima malisho kama zao la biashara. Dodoma upatikanaji wa majani ni mgumu hivyo, mtu anaweza kulima malisho kama zao la biashara akayakata akayaanika na kuyafunga katika mfumo wa bezi na kuwauzia wafugaji. Na soko lipo wazi kabisa kwa wafugaji na bei ni nzuri beli moja tunalipata kwa shilingi 4,000-...

WAFUGAJI DODOMA WASHAURIWA KUFUGA NG'OMBE KISASA

Image
  Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WAFUGAJI katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufuga kisasa ng’ombe wachache wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha. Amos Mwamyovellah, Mkurugenzi Mtendaji wa AJM&S Mwamyovellah Farm Production Kauli hiyo ilitolewa na Amos Mwamyovellah, Mkurugenzi Mtendaji wa AJM&S Mwamyovellah Farm Production alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea banda la mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maonesho ya Nanenane jijini Dodoma. Mwamyovellah alisema “ng’ombe hawa tumewaleta katika maonesho haya ya Nanenane ili kuwasaidia wenzetu wafugaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuweza kufuga kisasa. Wafugaji wanatakiwa kuwa na ng’ombe wa chache lakini wenye uwezo mkubwa kiuzalishaji”. Akiongelea chakula kinacholiwa na ng’ombe hao alisema kuwa wanakula chakula kizuri kilichoandaliwa kitaalam. “Chalula hiki kimechanganywa kitaalam kwa kutengeneza lishe bora kwa ng’ombe ili waweze kutupatia maziwa. Ng’ombe hawa tunakamua asubuhi, mc...

WAKAZI WA DODOMA WASHAURIWA KUPIMA UDONGO KABLA YA KILIMO

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WAKAZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya ya udongo ili kujua mahitaji ya virutubishi kwa udongo vitakavyosaidia kupata mazao mengi na bora. Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mjini, Yustina Munishi Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo mjini katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Yustina Munishi alipokuwa akiongelea umuhimu wa afya ya udongo kwa mkulima katika kuzalisha mazao bora na yenye tija. Munishi alisema kuwa kujua afya ya udongo ni muhimu sana kwa mkulima. “Napenda kuwataarifu kuwa kujua afya ya udongo ni muhimu sana kwa mkulima kabla ya kuanza kilimo alichokusudia. Kujua afya ya udongo kunamuwezesha mkulima kujua kiasi cha nyongo au tindikali kilichopo katika udongo. Ukijua afya ya udongo utajua ni zao gani uzalishe na linahitaji virutubisho gani na uweke mbolea ya aina gani na kwa kiasi gani ili uweze kupata mazao yaliyo bora. Hii ni muhimu kwa sababu watu wengi wanadanganyika kwa kuona udongo m...