WAFUGAJI DODOMA WASHAURIWA KUFUGA NG'OMBE KISASA
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI
WAFUGAJI
katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufuga kisasa ng’ombe
wachache wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha.
Amos Mwamyovellah, Mkurugenzi Mtendaji wa AJM&S Mwamyovellah Farm Production |
Kauli
hiyo ilitolewa na Amos Mwamyovellah, Mkurugenzi Mtendaji wa AJM&S
Mwamyovellah Farm Production alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
waliotembelea banda la mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maonesho
ya Nanenane jijini Dodoma.
Mwamyovellah
alisema “ng’ombe hawa tumewaleta katika maonesho haya ya Nanenane ili
kuwasaidia wenzetu wafugaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuweza kufuga
kisasa. Wafugaji wanatakiwa kuwa na ng’ombe wa chache lakini wenye uwezo mkubwa
kiuzalishaji”.
Akiongelea
chakula kinacholiwa na ng’ombe hao alisema kuwa wanakula chakula kizuri
kilichoandaliwa kitaalam. “Chalula hiki kimechanganywa kitaalam kwa kutengeneza
lishe bora kwa ng’ombe ili waweze kutupatia maziwa. Ng’ombe hawa tunakamua
asubuhi, mchana na jioni kulingana na wingi wa maziwa. Ng’ombe anatoa lita 36 za
maziwa na anafika lita 40 akiwa katika mzao wake wa kwanza na sasa ana kilo
780. Kama unavyomuona ni mpole na hana shida wakati wa kukamua” alisema Mwamyovellah.
Alisema
kuwa ng’ombe hao wanawapandisha kwa chupa ili kuweza kupata ubora wa ng’ombe.
Na mwendelezo wa ng’ombe hawa hivyo tunatumia ‘artificial insemination’. “Ng’ombe
huyu ana uwezo wa kuchangia 50% katika uzazi na dume akachangia 50%. Niwaombe
wafugaji wenzangu waweze kutembelea banda letu hapa Nanenane Halmashauri ya Jiji
la Dodoma tujifunze kwa pamoja tuweze kulima nyasi tuache kuzurura kwa ng’ombe
ili tuweze kufuga katika eneo dogo na tuweze kupata uzalishaji mkubwa kulingana
na ng’ombe ambao tunawafuga” alisema Mwamyovellah.
Mwananchi
aliyetembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Juma Alphonce alisema ni
mara yake ya kwanza kuona ng’ombe anayetoa maziwa makubwa kiasi hicho. “Haya
maonesho yanatusaidia kupata elimu ya ufugaji bora. Niwashauri wananchi wenye
nia ya kufuga ng’ombe kutembelea banda hili ili waweze kupata elimu bora ya
ufugaji” alisema Alphonce.
Maonesho
ya shughuli za wakulima Nanenane mwaka 2023 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo
“Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula”.
Amos Mwamyovellah, Mkurugenzi Mtendaji wa AJM&S Mwamyovellah Farm Production |
MWISHO
Comments
Post a Comment