WAFUGAJI KANDA YA KATI WASHAURIWA KULIMA MALISHO YA MIFUGO
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI
WAFUGAJI
katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufanya ufugaji wa ndani na
kulima malisho ya mifugo ili kujihakikishia kipato.
![]() |
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu |
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipotembelea Banda la Mifugo la Halmashauri
ya Jiji la Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
Mchomvu
alisema “tunahimiza wafugaji kufanya ufugaji wa ndani. Hivyo, ni muhimu mfugaji
alime malisho yake kwa ajili ya kujiongezea kipato na tija ya maziwa na nyama. Wakati
mwingine tunawafundisha ambao siyo wafugaji kulima malisho kama zao la
biashara. Dodoma upatikanaji wa majani ni mgumu hivyo, mtu anaweza kulima malisho
kama zao la biashara akayakata akayaanika na kuyafunga katika mfumo wa bezi na
kuwauzia wafugaji. Na soko lipo wazi kabisa kwa wafugaji na bei ni nzuri beli moja
tunalipata kwa shilingi 4,000-5,000”.
Alisema
kuwa Dodoma ina hali ya ukame ikipata mvua mara moja. “Kutokana na hali hii tunawafundisha
wafugaji kulima malisho kwa ajili ya kulisha ng’ombe wao wakiwa nyumbani. Teknolojia
hii tumeitoa ‘research’ Mpwapwa na Kongwa na katika vyuo vya mifugo
wanatufundisha jinsi ya kulima malisho ya mifugo na kuyahifadhi” alisema
Mchomvu.
MWISHO
Comments
Post a Comment