JIJI LA DODOMA LAJA NA TEKNOLOJIA YA NISHATI MBADALA MAONESHO YA NANENANE
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma imeanzisha teknolojia ya nishati mbadala ili kuondoa matumizi
ya kuni na mkaa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya kati.
Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George Joram |
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George
Joram alipokuwa akiongelea teknolojia ya nishati mbadala inayooneshwa katika
banda la mifugo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Joram
alisema “safari hii tumekuja na teknolojia ya nishati mbadala. Tunazalisha gesi
kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe. Kinyesi cha ng’ombe tunakikusanya kutoka
kwenye banda la ng’ombe tunachanganya kwa mchanganyo wa moja kwa moja.
Tunachukua kinyesi cha ng’ombe kwenye ndoo ya lita 20 na maji lita 20
tunachanganya na kuzalisha gesi”.
Alisema
kuwa baada ya saa 24 bacteria wanazalisha gesi inayoitwa Methane. “Badala ya
kutumia mkaa na nishati nyingine kama kuni, unaweza kutumia nishati mbadala ya
kutumia gesi ya kinyesi cha mifugo na kulinda na kutunza mazingira. Karibuni
sana Banda la Mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma mjionee wenyewe mambo ni
motomoto” alisema Joram kwa furaha.
Maonesho
ya shughuli za wakulima Nanenane mwaka 2023 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo
“Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula”.
MWISHO
Comments
Post a Comment