Posts

Jiji la Dodoma kutekeleza mradi wa urejeshaji taka

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya JUZA, Nasibu Kitabu kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Waste Solutions watambulisha mradi wa uchakataji na urejeshaji wa taka kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kupunguza kiwango cha taka zinazopelekwa katika Dampo la Chidaya. Aliyazungumza hayo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri na kusema kuwa taasisi hiyo imejikita katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira pamoja na kutoa elimu kwa vijana wanaofanya kazi ya kuzoa taka. “Kwasasa tupo katika Jiji la Dodoma na tumeungana na Global Waste Solutions kufanya hii kazi ili kupunguza kiasi kikubwa cha taka kwenda dampo ifikapo mwaka 2027. Yote hii ni kuweza kuifundisha jamii namna ya kutenganisha taka ili tuweze kuiokoa jamii yetu na changamoto zitokanazo na utunzaji na utupaji holela wa taka” alisema Kitabu. Aliongeza kuwa Jiji la Dodoma limekuwa kwa kasi na ndipo ilipo sura ya nchi. “Jili la Dodoma ni fahari ya watanzania, tumeona ni vem...

Wananchi Kata ya Kikuyu Kaskazini wafurahia huduma ya kujifungua Zahanati ya Kikuyu

Image
Na. Leah Mabalwe, KIKUYU KASKAZINI Kata ya Kikuyu Kaskazini yajivunia maboresho ya huduma za afya kwa kina mama jambo linalopunguza uwezekano wa vifo vya kina mama wajawazito na wakati wa kujifungua katika Zahanati ya Kikuyu. Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea Zahanati ya Kikuyu kujionea utoaji wa huduma katika jengo la wazazi ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kwa kipindi cha miaka minne kwenye Kata ya Kikuyu Kaskazini. Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kikuyu, Dkt. Azania Silliah alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, kwa kuwapatia shilingi 33,612,800 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa jengo la wazazi. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma aliwapatia shilingi 50,000,000 kwaajili ya umaliziaji wa jengo hilo. “Napenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Nipende kumshukuru Mbunge wetu, Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kwaajili ya kuhaki...

Mikopo ya asilimia 10 yawang’arisha wajasiriamali Makutupora

Image
Na. Nancy Kivuyo, MAKUTUPORA Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 yanufaisha makundi ya wanawake katika kujikwamua kiuchumi katika Kata ya Makutupora ikitajwa kuwa chachu ya kuinua maendeleo katika sekta ya kilimo, ufugaji na ujasiriamali. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na makundi ya wanawake waliopata mikopo ya asilimia 10 katika Kata ya Makutupora, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Makutupora, Andrew Boma alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kusimamia vema uwezeshaji wa wananchi kupata haki zao hasa kwa makundi maalum ambayo yamewezeshwa kupitia mikopo hiyo. “Sisi Kata ya Makutupora vikundi 20 vimepatiwa mkopo wa jumla ya shilingi 230,000,000. Vikundi vya wanawake ni 10, vijana saba na watu wenye ulemavu vitatu. Mpaka sasa wameweza kurejesha shilingi 159, 980,000 na bakaa inaendelea kulipwa na vikundi hivyo” alisema Boma. Aliongeza kuwa vikundi hivyo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali kama...

Kata ya Makutupora, kinara wa timu za michezo na ngoma za asili

Image
Na. Nancy Kivuyo, MAKUTUPORA Kata ya Makutupora yapongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita za kuboresha miundombinu ya michezo jambo iliyopelekea hamasa kwa wananchi kupenda kushiriki katika michezo kwaajili ya kuibua vipaji na kuboresha afya zao. Pongezi hizo zilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Matukupora Hamis Jigwa mbele ya waandishi wa habari waliofanya mazungumzo nae baada ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Alisema kuwa kwenye sekta ya michezo Kata ya Makutupora ina vikundi vya ngoma za asili ambavyo vimekuwa vikishiriki kwenye upokeaji wa Mwenge wa Uhuru na kushiriki mikutano ya kitaifa pamoja na timu za mpira wa miguu. “Hapa katani kwetu tupo vizuri, wananchi wa kata hii wanapenda michezo sana. Hata hii leo kuna mashindano yanaendelea, kama mtapata muda mtaona jinsi wananchi wa hapa wanavyojitokeza kwa wingi kushiriki katika michezo” alisema Jigwa. Akiongelea chachu ya hamasa ya michezo, alimtaja Rais, Dkt. Samia ...

Zabibu Hoteli Dodoma yajikita matumizi ya Nishati safi

Image
Na. Mussa Richard, TAMBUKARELI Kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha taasisi na sehemu zenye mkusanyiko wa watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia, imepokelewa na kufanyiwa kazi ipasavyo na uongozi wa Zabibu Hoteli, iliyopo Kata ya Tambukareli jijini Dodoma. Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Zabibu Hoteli, Mathew Gabriel, wakati akizungumza na vyombo vya Habari baada ya kutembelea hoteli hiyo ili kujionea matumizi ya nishati safi katika hoteli hiyo. “Zabibu Hoteli ni miongoni mwa taasisi ambayo imejizatiti kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye kila nyanja inayohusu mapishi. Nishati safi ya kupikia ni nzuri na ina faida nyingi kulinganisha na nishati zingine zinazochangia kwenye uchafuzi wa mazingira. Kwahiyo, niziombe sekta zote na watu binafsi wajikite katika matumizi ya nishati safi za kupikia kwasababu ni rahisi na salama” alisema Gabriel. Nae, Focus Mwenda, Mpishi Mkuu wa Zabibu Hoteli, alimshukur...

Wananchi Tambukareli wafurahia barabara miaka minne ya Rais Samia

Image
Na. Mussa Richard, TAMBUKARELI Diwani wa Kata ya Tambukareli jijini Dodoma, Juma Michael, amesema kuwa ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga barabara ya kiwango cha lami inayoanzia ‘ Shoppers’ hadi Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma kwa lengo la kupunguza msongamano na kurahisisha huduma ya usafiri. Diwani Michael, alisema hayo baada ya kutembelewa na waandishi wa habari ofisini kwake kwa lengo la kujionea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye Kata ya Tambukareli kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Kipindi cha nyuma tulikuwa na changamoto ya barabara, lakini tunaishukuru sana serikali imeweza kusikia kilio chetu na kuweza kutujengea barabara yenye kiwango cha lami. Barabara ambayo imekuja kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla, kwasababu hapo awali wafanyabiashara walikuwa wana shindwa jinsi ya kufikisha bidhaa katika ...

Bado siku 18 Mwenge wa Uhuru uingie Jiji la Dodoma

Image
 

Kheri ya Kumbukizi ya Karume

Image
 

Zimebaki Siku 19 Kupokea Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma

Image
 

Global Affairs Canada yafurahishwa na utekelezaji wa Mradi wa AHADI katika Kata ya Chamwino

Image
  Kata ya Chamwino, imepokea ugeni kutoka Global Affairs Canada ukiongozwa na Mary Harasym aliyeambatana na Zahra Popatia ambao ni wafadhili wa mradi wa AHADI na kueleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo. Lengo la ziara hiyo ni kufanya tathimini na kujionea kwa macho namna mradi unavyotekelezwa hususan utoaji wa elimu kuhusu maswala ya Afya ya uzazi kwa vijana wa Kata ya Chamwino. Kwa upande ‘Promoter’ wa mradi, Khadija Ally alitoa maelezo ya kina kuhusu shughuli zinazofanyika na mafanikio yaliyopatikana kwa vijana kushiriki kwenye mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kuhusu maswala Afya ya uzazi, kujikinga dhidi ya mimba zisizotarajiwa na kuwa na mipango bora ya maisha ya baadae pamoja na kuwajengea uwezo wa kuwa na shughuli za kuingiza kipato. Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, kwa niaba ya Diwani aliwashukuru wageni hao kwa kuitembelea Kata ya Chamwino na kusema kuwa mradi wa AHADI ni kielelezo kizuri cha ushirikiano baina ya kata yake...