Kata ya Makutupora, kinara wa timu za michezo na ngoma za asili
Na. Nancy Kivuyo, MAKUTUPORA
Kata
ya Makutupora yapongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita za kuboresha
miundombinu ya michezo jambo iliyopelekea hamasa kwa wananchi kupenda kushiriki
katika michezo kwaajili ya kuibua vipaji na kuboresha afya zao.
Pongezi hizo zilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Matukupora Hamis Jigwa mbele ya waandishi wa habari waliofanya mazungumzo nae baada ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.
Alisema
kuwa kwenye sekta ya michezo Kata ya Makutupora ina vikundi vya ngoma za asili ambavyo
vimekuwa vikishiriki kwenye upokeaji wa Mwenge wa Uhuru na kushiriki mikutano
ya kitaifa pamoja na timu za mpira wa miguu. “Hapa katani kwetu tupo vizuri,
wananchi wa kata hii wanapenda michezo sana. Hata hii leo kuna mashindano
yanaendelea, kama mtapata muda mtaona jinsi wananchi wa hapa wanavyojitokeza
kwa wingi kushiriki katika michezo” alisema Jigwa.
Akiongelea
chachu ya hamasa ya michezo, alimtaja Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ni
kielelezo na chachu ya hamasa ya michezo. “Kama mnavyoona ndugu waandishi kuna
mashindano yanaendelea hapa, kupitia kampuni iitwayo JBM Ramadhani Cup ambayo
yana zawadi nzuri na yana lengo la kuunganisha wananchi na kujenga afya ya
mwili” aliongeza Jigwa.
Alimalizia
kwa kusema kuwa Kata ya Makutupora ipo mbioni kuandaa mashindano kwaajili ya kuhakikisha
vijana wanaonesha vipaji vyao. “Mashindano hayo tutaweka vituo viwili na bingwa
wa kila kituo atapata zawadi ya mbuzi na baadae vile vituo viwili bingwa wa
kituo ‘A’ na bingwa wa kituo ‘B’ watacheza mechi mbili nyumbani na ugenini na
bingwa atapata mbuzi. Kwahiyo, sisi kwetu suala la michezo tumelipa kipaumbele
sana” alisisitiza Jigwa.
Nae,
mwananchi wa Kata ya Makutupora, Julias Twaja aliipongeza serikali kwa msukumo
wa kuboresha eneo la michezo kwasababu linawafanya watoto na vijana
kuchangamkia fursa ya kuvumbua vipji vyao. “Michezo katika miaka ya karibuni
imekuwa ni ajira nzuri sana kwa watoto na vijana wetu. Ofisi ya kata inafanya
vizuri katika kuhamasisha michezo, tuna timu nyingi sana ukanda huu, tunaamini
kwa siku zijazo Makutupora tutang’ara katika sekta ya michezo kiujumla”
alipongeza Twaja.
MWISHO
Comments
Post a Comment