Zabibu Hoteli Dodoma yajikita matumizi ya Nishati safi
Na. Mussa Richard, TAMBUKARELI
Kampeni
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya
kuhakikisha taasisi na sehemu zenye mkusanyiko wa watu zaidi ya 100 kutumia nishati
safi ya kupikia, imepokelewa na kufanyiwa kazi ipasavyo na uongozi wa Zabibu
Hoteli, iliyopo Kata ya Tambukareli jijini Dodoma.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Zabibu Hoteli, Mathew Gabriel, wakati akizungumza na vyombo vya Habari baada ya kutembelea hoteli hiyo ili kujionea matumizi ya nishati safi katika hoteli hiyo.
“Zabibu
Hoteli ni miongoni mwa taasisi ambayo imejizatiti kwenye matumizi ya nishati safi
ya kupikia kwenye kila nyanja inayohusu mapishi. Nishati safi ya kupikia ni
nzuri na ina faida nyingi kulinganisha na nishati zingine zinazochangia kwenye
uchafuzi wa mazingira. Kwahiyo, niziombe sekta zote na watu binafsi wajikite
katika matumizi ya nishati safi za kupikia kwasababu ni rahisi na salama” alisema
Gabriel.
Nae,
Focus Mwenda, Mpishi Mkuu wa Zabibu Hoteli, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuanzisha kampeni ya
matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. “Sisi kama Zabibu Hoteli, tunaunga
mkono juhudi za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhimiza matumizi ya nishati
safi ya kupikia kwenye shughuli zote za mapishi. Kiukweli, nishati safi ni
nzuri kwasababu inaokoa muda na ni rahisi pia kupatikana na kutumia” alisema
Mwenda.
Kwa
upande wake, Juma Michael, Diwani wa Kata ya Tambukareli, akatoa wito kwa
wananchi kuhakikisha wanatumia nishati safi ili kusaidia kutunza mazingira. “Nitoe
rai kwa jamii inayotuzunguka kuhakikisha inantumia nishati safi ya kupikia. Kwa
sababu hii ni kampeni ya kitaifa, dhima ya Rais wetu ni kuhakikisha kila
mwananchi anatumia nishati safi na salama ili mazingira ya nchi yetu yawe bora
na afya za wananchi ziwe bora pia” alimalizia Michael.
MWISHO
Comments
Post a Comment