Global Affairs Canada yafurahishwa na utekelezaji wa Mradi wa AHADI katika Kata ya Chamwino
Kata
ya Chamwino, imepokea ugeni kutoka Global Affairs Canada ukiongozwa na Mary
Harasym aliyeambatana na Zahra Popatia ambao ni wafadhili wa mradi wa AHADI na
kueleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Lengo
la ziara hiyo ni kufanya tathimini na kujionea kwa macho namna mradi
unavyotekelezwa hususan utoaji wa elimu kuhusu maswala ya Afya ya uzazi kwa
vijana wa Kata ya Chamwino.
Kwa
upande ‘Promoter’ wa mradi, Khadija Ally alitoa maelezo ya kina kuhusu shughuli
zinazofanyika na mafanikio yaliyopatikana kwa vijana kushiriki kwenye mafunzo
yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kuhusu maswala Afya
ya uzazi, kujikinga dhidi ya mimba zisizotarajiwa na kuwa na mipango bora ya
maisha ya baadae pamoja na kuwajengea uwezo wa kuwa na shughuli za kuingiza
kipato.
Afisa Mtendaji
wa Kata ya Chamwino, kwa niaba ya Diwani aliwashukuru wageni hao kwa
kuitembelea Kata ya Chamwino na kusema kuwa mradi wa AHADI ni kielelezo kizuri
cha ushirikiano baina ya kata yake na Canada.
Mradi
wa AHADI unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya shirika la World Vision na TAHEA.
MWISHO
Comments
Post a Comment