Wananchi Kata ya Kikuyu Kaskazini wafurahia huduma ya kujifungua Zahanati ya Kikuyu
Na. Leah Mabalwe, KIKUYU KASKAZINI
Kata
ya Kikuyu Kaskazini yajivunia maboresho ya huduma za afya kwa kina mama jambo
linalopunguza uwezekano wa vifo vya kina mama wajawazito na wakati wa
kujifungua katika Zahanati ya Kikuyu.
Akiongea
na waandishi wa habari waliotembelea Zahanati ya Kikuyu kujionea utoaji wa
huduma katika jengo la wazazi ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya
maendeleo iliyotekelezwa na serikali kwa kipindi cha miaka minne kwenye Kata ya
Kikuyu Kaskazini.
Mganga
Mfawidhi wa Zahanati ya Kikuyu, Dkt. Azania Silliah alimshukuru Mbunge wa Jimbo
la Dodoma Mjini, kwa kuwapatia shilingi 33,612,800 kwa ajili ya kuanzisha
ujenzi wa jengo la wazazi. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma aliwapatia shilingi
50,000,000 kwaajili ya umaliziaji wa jengo hilo.
“Napenda
kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa kuona umuhimu wa kusogeza
huduma za afya karibu na wananchi. Nipende kumshukuru Mbunge wetu, Anthony
Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kwaajili ya kuhakikisha wazazi wanapata huduma
nzuri wakati wa kujifungua kwa kutoa fedha ya uanzishaji wa mradi wa ujenzi wa
Zahanati ya Kikuyu. Pia namshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kuunga
mkono jitihada za mbunge wetu” alishukuru Dkt. Silliah.
Mwananchi Johari Issa alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kujenga jengo la wazazi katika Zahanati ya Kikuyu. “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutujengea jengo la wazazi la kujifungulia pamoja na huduma ya mama na mtoto, kwasababu hapo awali tulikuwa hatuna kabisa jengo la wazazi. Tulikuwa tukitembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma ya kujifungua kutoka sehemu moja kwenda nyingine na tulikuwa tunapata shida kwasababu muda mwingine tunatembea usiku kwaajili ya kufuata huduma. Kwa hivi sasa hatupati tena adha ya kutembea umbali mrefu kwasababu huduma imesogezwa karibu” alishukuru Issa.
Kwa
upande wake, Imelda Kessa aliipongeza serikali kwa kuwapelekea vifaa vya kisasa
kwaajili ya kujifungulia katika jengo la wazazi. “Naishukuru serikali ya awamu
ya sita kwa kutuwekea vifaa vya kisasa, katika zahanati yetu ya Kikuyu. Hii zahanati
ni ya mfano kwasababu kuna vifaa na huduma nzuri zinazotolewa hasa wazazi
kujifungua. Zahanati ina wauguzi wabobezi katika kazi yao” alipongeza Kessa.
MWISHO
Comments
Post a Comment