Wananchi Tambukareli wafurahia barabara miaka minne ya Rais Samia
Na. Mussa Richard, TAMBUKARELI
Diwani
wa Kata ya Tambukareli jijini Dodoma, Juma Michael, amesema kuwa ndani ya miaka
minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan amejenga barabara ya kiwango cha lami inayoanzia ‘Shoppers’ hadi Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma kwa lengo la kupunguza
msongamano na kurahisisha huduma ya usafiri.
Diwani Michael, alisema hayo baada ya kutembelewa na waandishi wa habari ofisini kwake kwa lengo la kujionea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye Kata ya Tambukareli kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kipindi
cha nyuma tulikuwa na changamoto ya barabara, lakini tunaishukuru sana serikali
imeweza kusikia kilio chetu na kuweza kutujengea barabara yenye kiwango cha
lami. Barabara ambayo imekuja kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara, wajasiriamali
na wananchi kwa ujumla, kwasababu hapo awali wafanyabiashara walikuwa wana
shindwa jinsi ya kufikisha bidhaa katika maeneo yetu kutokana na ubovu wa
miundombinu ya barabara. Lakini kwasasa, wanachi wa Kata ya Tambukareli
wanapata mahitaji yao yote kwa uharaka na kwa wakati kutokana na ubora wa
miundomninu” alisema Michael.
Nae,
Daudi Jackson, mwananchi Kata ya Tambukareli, akaishukuru Serikali kwa
kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo. “Ujenzi wa barabara hii
umekuwa na manufaa makubwa kwa sisi wananchi wa Kata ya Tambukareli, kwa sababu
kwasasa tunaweza kusafirisha bidhaa zetu kutoka mjini kuja Tambukareli kwa
haraka. Pia, tunaweza kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, pia barabara
hii inasaidia kufika kwa haraka kwa magari ya dharura pindi linapotokea janga kama moto au kuna mgonjwa
anaehitajika kufika hospitali kwa haraka” alisema Michael.
MWISHO
Comments
Post a Comment