Posts

“Maandalizi Uandikishaji Uchaguzi Serikali za Mitaa yamekamilika” Dkt. Sagamiko

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko amesema kuwa maadalizi katika uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika kwa asilimia mia moja. Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akifafanua jambo Dkt. Sagamiko alitoa kauli hiyo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma. Msimamizi huyo alisema kuwa maandalizi katika uandikishaji kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika. Vifaa vyote vimefika na rasilimali fedha, Rais amewezesha kwa asilimia mia moja. “Kwa maandalizi, tupo timamu. Matamanio yetu tukamilishe zoezi la uandikishaji katika siku tatu” alisisitiza Dkt. Sagamiko. Aidha, aliwapongeza watumishi na wananchi waliojitokeza kwa wingi kushiriki ‘jogging’ n...

Madiwani Jiji la Dodoma wapo tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapo tayari kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa asilimia 100. Mwakilishi wa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Daud Mkhandi alipotoa salamu katika Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Daud Mkhandi alipotoa salamu katika Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma. Mkhandi ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira alisema “kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, tupo tayari kushiriki zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa asilimia 100. Waheshimiwa Madiwani tupo tayari kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha. Waheshimiwa Madiwani tupo tayari kuwahamasish...

RC Dodoma atamani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanikiwe kwa 100%

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MKOA wa Dodoma unatamani kuona zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa linafanikiwa kwa asilimia mia moja kwa kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri wakati akifungua Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Shule ya Sekondari Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri wakati akifungua Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma anatufundisha kujitambua na kujithamini kupitia kaulimbiu yake isemayo ‘Dodoma Fahari ya Watanzania’. Pia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi mkubwa katika Dodoma ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa Msalato. Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko na ujen...

Twende Butiama kupambana na ujinga, umasikini na maradhi Jiji la Dodoma

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA MAKULU Waendesha baiskeli wamuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Nyerere kwa lengo la kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni maradhi, umasikini na ujinga kwa kugawa madawati 100 katika Shule ya Msingi Dodoma Makulu iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.   Mwenyekiti wa msafara Twende Butiama Gabriel Landa, alisema kuwa msafara huo una lengo la kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo kwasababu Mwl. Julius Nyerere alitumia chombo cha baiskeli wakati alipokuwa mwalimu na hata alipoacha uwalimu na kuanza harakati za kupigania uhuru na mambo mbalimbali alitumia baiskeli. Mwalimu Nyerere pia aliwahi kusafiri kwa kuendesha baiskeli kutoka Dar-es-Salaam hadi Arusha, aliongeza. Msafara huo umewaunganisha watu wa nchi mbalimbali kwa kuonesha Mwalimu Nyerere alikuwa sio mbinafsi bali mpenda umoja. “Wengi wanaotuona barabarani wanahisi haya ni mashindano ila haya sio mashindano bali ni msafara wa kawaida ambao tunaendesha baiskeli kwa mwendo wa upendo am...

Twende Butiama wakabidhi Madawati 100 SM Dodoma Makulu

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA MAKULU   Watu wasiopungua 90 washiriki kwenye msafara wa Twende Butiama wakiendesha baiskeli kutoka Dar-es-Salaam na kwenda Butiama kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Nyerere waliwasili jijini Dodoma katika Shule ya Msingi Dodoma Makulu na kugawa madawati 100 na kushiriki zoezi la kupanda miti.   Msafara huo ulianza safari tarehe 30 Septemba kutoka Dar-es-Salam na unatarajiwa kufika Butiama tarehe 13 Oktoba, 2024 ukidhaminiwa na Vodacom pamoja na Benki ya Stanbic walikabidhi madawati 100 na kupanda miti katika Shule ya Msingi Dodoma Makulu.   Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya aliupokea msafara huo wa Twende Butiama na alisema kuwa, upandaji miti unaunga falsafa ya kutunza Mazingira. Alisema kuwa utoaji wa madawati shuleni unaugana na falsafa ya Mwl. Julius Nyerere ya kuangamiza maadui watatu wa maendeleo ikiwemo ujinga, umasikini na maradhi.   Alisema kuwa, kitendo wanachofanya ni kizuri kwa Tanz...

Naibu Meya Chibago afurahia Kampeni ya Upandaji Miti Dodoma

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA MAKULU Naibu Meya wa Halmashauri Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago amefarijika na kampeni ya upandaji miti inayofanywa na wanariadha wanaotumia baiskeli katika kuzienzi falsafa za Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere ya kupambana na adui wa maendeleo kwa kuondoa ujinga, maradhi na umasikini. Naibu Meya wa Halmashauri Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago akielezea kufurahia kampeni ya upandaji miji  Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa, Kaspar Mmuya katika zoezi la upandaji miti na ugawaji madawati katika Shule ya Msingi Dodoma Makulu, jijini Dodoma lililofanywa na wanariadha kutokea Dar es Salaam wakielekea Butiama. Chibago alisema kuwa amefarijika sana na kampeni ya wanariadha hao wa kuendesha baiskeli, upandaji miti ikiwa ni falsafa moja wapo ya kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere katika falsafa zake tatu za kupambana na maadui wa maendeleo ambao ni ujinga, umaskini na maradhi. “Jiji la Dodoma tumefarijika sana na ka...

Vijana wajitokeze kujiandikisha Daftari la kudumu la wapiga kura

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA VIJANA katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi leo kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili watumie haki yao ya kikatiba ya kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani katika uchaguzi mkuu ujao. Ushauri huo ulitolewa na Mwandishi wa Habari Mwandamizi kutoka Uhondo TV, Fadhili Komba muda mfupi baada ya kujiandikisha katika kituo cha Zahanati ya Reli kilichopo Kata ya Tambukareli, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Komba alisema kuwa vijana wanawajibu wa kujitokeza kwa wingi ili kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia. “Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya uandikishaji kwa ajili ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma muda bado upo wa kutosha. Kijana mwenzangu haujachelewa, wahi sasa ukajiandikishe au kuboresha taarifa zako. Tukumbuke vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa” alisema Komba. Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukihusi...

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA AKIWAAPISHA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA NA MITAA

Image
 

SEMINA YA MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA NA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA

Image
 

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA AKIWAAPISHA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA NA MITAA

Image