Vijana wajitokeze kujiandikisha Daftari la kudumu la wapiga kura
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
VIJANA katika Halmashauri
ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi leo kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura ili watumie haki yao ya kikatiba ya kumchagua Rais,
Wabunge na Madiwani katika uchaguzi mkuu ujao.
Ushauri huo ulitolewa na Mwandishi wa Habari Mwandamizi kutoka Uhondo TV, Fadhili Komba muda mfupi baada ya kujiandikisha katika kituo cha Zahanati ya Reli kilichopo Kata ya Tambukareli, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Komba alisema
kuwa vijana wanawajibu wa kujitokeza kwa wingi ili kutumia haki yao ya kikatiba
na kidemokrasia. “Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya uandikishaji kwa ajili ya
kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma
muda bado upo wa kutosha. Kijana mwenzangu haujachelewa, wahi sasa
ukajiandikishe au kuboresha taarifa zako. Tukumbuke vijana ndiyo nguvu kazi ya
taifa” alisema Komba.
Zoezi la
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma ukihusisha usajili wa wapiga kura wapya waliotimiza umri wa miaka 18,
kurekebisha, kubadili taarifa au kuhama kituo chini ya kaulimbiu isemayo “Kujiandikisha
kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora linafikia kilele chake leo”.
MWISHO
Comments
Post a Comment