“Maandalizi Uandikishaji Uchaguzi Serikali za Mitaa yamekamilika” Dkt. Sagamiko
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko amesema kuwa maadalizi katika
uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika kwa
asilimia mia moja.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akifafanua jambo
Dkt. Sagamiko alitoa kauli hiyo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Msimamizi huyo alisema kuwa maandalizi katika
uandikishaji kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika. Vifaa vyote
vimefika na rasilimali fedha, Rais amewezesha kwa asilimia mia moja. “Kwa
maandalizi, tupo timamu. Matamanio yetu tukamilishe zoezi la uandikishaji
katika siku tatu” alisisitiza Dkt. Sagamiko.
Aidha, aliwapongeza watumishi na wananchi waliojitokeza
kwa wingi kushiriki ‘jogging’ na Bonanza la kuhamasisha umma kushiriki mchakato
wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Pia alipongeza maandalizi mazuri ya Bonanza
hilo kubwa la kihistoria katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki
machakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 lilikuwa na michezo ya riadha,
mbio za magunia, kukimbiza kuku, kukimbia na glasi, kuvuta Kamba, kukimbia na yai
kwenye kijiko, mpira wa miguu, mpira wa mikono, bao, drafti, karata, kunywa
soda na kukuna nazi wanaume chini ya kaulimbiu isemayo “Serikali za Mitaa,
Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”.
.
MWISHO
Comments
Post a Comment