Dodoma yakusanya Sh. Milioni 5.6 ukiukaji wa sheria za usafi

Na. Mwandishi wetu, MSALATO

 

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekusanya shilingi milioni 5.66 kutokana na hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wananchi na wafanyabiashara waliokiuka sheria ndogo za usafi wa mazingira.

 


Fedha hizo zimepatikana baada ya ukaguzi uliofanyika katika maeneo ya makazi, biashara na taasisi, ambapo kaya 2,675 na maeneo 1,582 ya biashara yalikaguliwa na kutolewa kwa mrundikano wa taka katika maeneo mbalimbali ya jiji.

 

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za usafi wa mazingira, Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu, Mkana Mkana alisema kuwa hatua hizo zinatekelezwa kwa mujibu wa maagizo ya serikali.

 

“Hatua hizi ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya viongozi wa serikali ya kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika kwa kuendelea na kwamba wanaokiuka sheria wanachukuliwa hatua stahiki,” alisema Mkana.

 

Aidha, aliongeza kuwa pamoja na hatua hizo, halmashauri imeeleza kuwa bado inakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wananchi na wafanyabiashara kutofuata kanuni za usafi, huku baadhi ya kata na mitaa zikiwa hazina wazabuni wa uondoshaji taka.

 

Halmashauri imesema itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watakaokiuka kanuni za usafi, huku ikiimarisha elimu kwa umma na kupanga wafanyabiashara ndogondogo katika maeneo rasmi yaliyotengwa kwa shughuli za biashara.

MWISHO

 

 

Comments

Popular Posts

Polisi Kata waungana zoezi la Usafi wa Mazingira Dodoma

Kata ya Matumbulu wanufaika na Mil. 14.7 Maadhimisho ya Samia Day

Samia Day 2026 yaibua vipaji vya michezo Kata ya Matumbulu