VYOMBO VYA HABARI VISIIACHIE DCEA PEKE YAKE VITA DAWA ZA KULEVYA- DK. RIOBA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kushirikiana na Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) katika mapambano ya dawa hizo, kwani vita hiyo ni ngumu hivyo DCEA haitakiwi kuachwa peke yake. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari Tanzania( TBC) Dk.Ayub Rioba akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya( DCEA) kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu vita dhidi ya dawa za kulevya Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba, wakati akitoa mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kupambana na dawa za kulevya kwenye semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na DCEA. Amesema vyombo vya habari vina wajibu wa kushirikiana na DCEA katika mapambano ya dawa za kulevya ikiwemo vile vya maudhui (mitandaoni) kwani mchango mkubwa kwenye vita hiyo. Dk. Rioba, amesema tafiti zinaonesha biashara...