WAZIRI SILAA APANIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI JIJI LA DODOMA
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema
Wizara yake itahakikisha kero zote za migogoro ya ardhi zinakwisha katika
Jijini la Dodoma ikiwa ni hatua muhimu ya utekelezaji rasmi maagizo
ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
![]() |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akimsikiliza mwananchi katika Kliniki ya Ardhi Kata kwa Kata inayoendelea jijini Dodoma |
Akiongea na wananchi waliofika katika Kliniki ya Ardhi Waziri Silaa alisema kuwa lengo la kuweka kambi katika Ofisi
ya Kamshina Msaidizi wa Ardhi wa Jiji la Dodoma ni kuhakikisha wanawahudumia
wananchi ipasavyo.
Waziri Silaa aliwaaambia wananchi waliofika kupata huduma katika
kliniki hiyo kuwa atakuwa akifanya nao mazungumzo kila baada ya kumaliza ratiba
ya bunge ili kujionea mwenyewe kero zinazowakabili wananchi hao.
Mwananchi Foime Yohana alitoa dukuduku lake kwa Waziri Silaa baada ya kuwa
na kero ya muda mrefu ya kuvamiwa na kuchukuliwa eneo lake nakuomba Waziri huyo
kusaidia ili aweze kupata haki yake.
Akiongea na vyombo vya habari wakati zoezi la kuhudumia wananchi
likiendelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi
Anthony Sanga alisema kuwa Kliniki ya Ardhi inayoendelea kwa wiki mbili jijini
Dodoma, itakuwa mwarobaini wa changamoto nyingi za ardhi zinazowakabili
wananchi wengi wa jiji hilo.
Mhandisi Sanga alisema kuwa baada ya kupokea maagizo ya Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi tayari ameanza kuyafanyia kazi yeye
pamoja na watendaji wa Ardhi ikiwa ni kutatua changamoto za Ardhi
zinazowakabili wananchi pamoja na ugawaji wa hatimiliki za Ardhi.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu alisema kuwa Jiji la Dodoma
ndio lenye changamoto nyingi za mgogoro ya Ardhi na wizara imejipanga
kikamilifu kwa kupiga kambi ya wiki mbili ili kuhakikisha changamoto zote za
Ardhi Mkoa wa Dodoma zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili wananchi wapate haki
zao.
![]() |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga (wa kwanza kushoto) akikabidhi Hati |
“Kliniki ya Ardhi kwa sasa iko Dodoma na niendelevu kwa mikoa
yote, pia Wizara inakusudia kuweka mifumo rahisi ya kutoa huduma kwa wananchi
ikiwemo kufunga kamera katika ofisi za utoaji huduma ili kuepuka mianya ya
ukiukwaji wa sheria” alisema Mhandisi Sanga.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa mchakato
wa kuanzisha kwa Program tumishi yaani Ardhi App ili kurahisha wananchi kupata
huduma popote pale nchini kwa njia ya mtandao ikiwemo huduma ya ulipaji wa
pango ya Ardhi.
MWISHO
Comments
Post a Comment