PROF. MWAMFUPE APONGEZA UFANISI KLINIKI YA ARDHI DODOMA
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mwenyekiti
wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis
Mwamfupe amepongeza ufanisi wa Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini hapa na
kusema ni mafanikio makubwa.
![]() |
Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akitoa pongezi kwa Kliniki ya Ardhi Jiji la Dodoma |
Pongezi
hizo alizitoa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya kwanza
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Prof.
Mwamfupe ambae ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “kniliki hiyo
ni muendelezo wa mafanikio katika sekta ya Ardhi. Jana pekee zimetolewa hati
217, zikijumuisha maombi yaliyopokelewa papo kwa hapo. Tuendelee kutoa
mapendekezo ya namna ya kuboresha kliniki hii”.
Katika
hatua nyingine, Prof. Mwamfupe ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Halmashauri
ya Jiji la Dodoma ya Fedha na Utawala alimteua Diwani wa viti maalum, Rosemary
Nitwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala.
“Waheshimiwa madiwani, mtakumbuka Mheshimiwa Grace
Milinga alikuwa mmoja wetu hapa akiwa Diwani na alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha
na Utawala na alijiuzuru nafasi hiyo. Naomba mridhie kuteuliwa kwa Mheshimiwa Rosemary
Nitwa kuziba pengo hilo” aliomba Prof. Mwamfupe na madiwani kuridhia.
![]() |
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakifuatilia mkutano |
MWISHO
Comments
Post a Comment