Na. Veronica John, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule awapongeza wafugaji kwa kujitokeza kwa wingi katika shindano la Paredi ya Mifugo Kitaifa 2025 ambalo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1-8 Agosti. Akizungumza na wafugaji, Senyamule alisema kuwa ameshuhudia mabadiliko na maboresho makubwa katika shughuli za mifugo ambapo hapo awali ilifanyika kikanda na sasa yameenda kimataifa. Alisema kuwa mashindano hayo kufanyika sehemu nyingi duniani yakiwa na lengo la kutambua mchango na juhudi za wafugaji katika kuchangia maendeleo ya taifa na ya mtu mmoja mmoja. “Maonesho haya huongeza ari kwa wananchi katika kuinua hadhi ya uzalishaji na tija kwa kutumia teknolojia mpya zilizoboreshwa katika shughuli za ufugaji ili kukidhi mahitaji ya soko. Na nimearifiwa kuwa maonesho na mashindano haya yaliasisiwa na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010 katika siku ya kilele cha sherehe za maonesho ya Nanenane Dodoma” a...
Comments
Post a Comment