Tanzania na Uingereza zakubali kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Madini
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Marianne Young amekutana na
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu sekta ya
madini nchini Tanzania na fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya Uingereza na
Tanzania.
Mkutano huo ulijadili kuhusu uwekezaji, uongezaji wa thamani, na kuhakikisha sekta hiyo inachangia katika ukuaji wa uchumi unaoshirikisha wote.
Tanzania na Uingereza zitaendelea kushirikiana
katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili ili kudumisha ustawi wa
mataifa yote mawili.
Comments
Post a Comment