Hai DC yajifunza kuimarisha usafi na usimamizi wa taka Jiji la Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Viongozi na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamejifunza mbinu za usafi wa mazingira na usimamizi wa taka katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kuboresha usafi na kuimarisha utunzaji wa mazingira. Ziara hiyo ilijumuisha kutembelea Dampo la Chidaya lililopo Jiji la Dodoma, ambako wajumbe walijifunza taratibu za upokeaji, utenganishaji, usafirishaji na uhifadhi wa taka. Afisa Uendeshaji wa Dampo, Elias Banyikila alisema kuwa Dodoma huzalisha wastani wa tani 594 za taka kwa siku, huku tani 392 zikipokelewa d Dampo la Chidaya na tani 54 zikirejelezwa. Alisema kuwa dampo hilo lina ukubwa wa ekari 48, lakini takribani ekari 12 pekee ndizo zinazotumika, likiwa na miundombinu inayojumuisha uzio, ofisi, mizani, nyumba za walinzi na mitambo. “Dampo hili linapokea taka za kawaida kutoka majumbani na masokoni, lakini taka hatarishi, ikiwemo za hospitalini, hushughulikiwa kwa utaratibu maalumu,”...
Comments
Post a Comment