Zahanati ya Chihoni Medical Center yazinduliwa Dodoma, wagonjwa 1,313 wahudumiwa
Na. Mwandishi wetu, ZUZU Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amezindua rasmi Zahanati ya Chihoni Medical Center iliyopo katika Kata ya Nala jijini Dodoma, kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kupunguza changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu. Alisema uwekezaji huko ni muhimu katika Jiji la Dodoma kulingana na Dira ya Taifa ya 2050, huku akiwaasa wananchi kutumia vizuri huduma ambazo wawekezaji wamezisogeza karibu nao “Kuanzishwa kwa zahanati hii ni hatua muhimu katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Zuzu na maeneo jirani. Serikali inaendelea kuhimiza juhudi za wadau binafsi kuwekeza katika sekta ya afya ili kusogeza huduma karibu na wananchi, kupunguza umbali wa kufuata matibabu na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za afya kwa wakati.” alisema Shekimweri Uzinduzi huo umefanyika Novemba 20, 2026, ukishuhudiwa na mamia ya wakazi wa eneo la Nala na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa ...
Comments
Post a Comment