Timu ya Jiji la Dodoma yatakiwa kudumisha nidhamu mashindano ya SHIMISEMITA
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
Wachezaji
wanaojiandaa kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA watakiwa kuwa na malengo
makubwa, nidhamu na ari ili kuweza kupata ushindi.
Hayo aliyasema Mwenyekiti wa SHIMISEMITA Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Gerald Ruzika wakati wa kikao chake na washiriki wa timu ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutaho wa halmashauri jijini Dodoma.
Aliseama
kuwa malengo yetu ni kupambania nafasi ya juu. “Mnakwenda kuiwakilisha
Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Muwe na malengo ya ushindi na mkapambane
kuurudisha ubingwa kama mlivyofanya mwaka jana. Fanyeni mazoezi kwa bidii, muwe
na nidhamu na mshikamano ili mkaandike historia nyingine ya mafanikio,” alisema
Dkt. Ruzika.
Aidha,
aliwasisitiza washiriki kuongeza juhudi katika mazoezi na kuzingatia maelekezo
ya makocha wao ili kuhakikisha wanakuwa katika kiwango bora kitakachowawezesha
kufanya vizuri na kuipeperusha vema bendera ya Jiji la Dodoma.
Kwa
upande wake, Nahodha wa Mpira wa Pete, Mwajuma Banyasa, alisema kuwa maandalizi
yanaendelea vizuri na kila mshiriki ameonesha ari ya ushindani, jambo
linalowapa imani ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo. “Tunafanya mazoezi
kwa bidii na maandalizi yetu ni mazuri. Tuna imani kubwa ya kurudi na ushindi.
Kwa wapinzani wetu nawaambia tu, tumejipanga vya kutosha na ushindi ni wa Jiji
la Dodoma” alisema Banyasa.
Comments
Post a Comment